MMENYUKO MKALI WA MZIO ■ Baadhi ya watu hupatwa na hali hatari inayoweza kuhatarisha maisha baada ya kuumwa na mdudu, kula baadhi ya vyakula kama vile njugu au samaki, au kutumia madawa fulani. ■ Mshtuko huu unaotokana na mmenyuko mkali au mjibizo mbaya wa mzio ‘’allergic reaction’’ huitwa ‘’anaphylactic shock’’ kitaalamu. ■ Dalili za ‘’anaphylactic shock’’ huanza dakika kadhaa baada ya kuumwa na mdudu au kula kitu ambacho ana mzio nacho, hii husababisha shinikizo la damu kushuka haraka sana na njia ya hewa kuanza kuziba kwa kasi. ■ Dalili nyingine ni pamoja na kukorota; kuvimba macho na uso, midomo na ulimi; kupata vipele vyekundu vinavyosambaa mwili mzima; kutapia hewa kwa sababu hewa inashindwa kuingia ndani; na woga mkubwa. Kuna hatari kubwa ya kupata mshtuko na mtu kupoteza fahamu. □ JIFUNZE ZAIDI NINI CHA KUFANYA 👉 https://wikielimu.com/mmenyuko-mkali-wa-mzio/ #wikielimu #afya #afyayako https://www.instagram.com/p/COLnXPHLwtL/?igshid=vnie86zxdr7y













