TBT 1999 Erith, Kent. Maisha ni pamoja na kumbukizi ya matukio yaliyobadilisha mwelekeo wa uzoefu wa maisha yangu duniani. Kila tukio katika maisha hunifunza jambo fulani. Mafunzo mengine hukubadilisha kabisa mwelekeo wa maisha yako. Unatakiwa kutambua kuwa kila jambo hutokea kwa sababu fulani, na ni muhimu kuchukulia kila jambo kama shule na kujifunza sababu ya tukio husika. Matukio ya ugonjwa wa corona umeifanya dunia kubadilika na kufanya mambo ambayo hakuna aliyetegemea. Nani alifikiri kuna siku ndege zote za usafiri wa abiria duniani zingelala chini badala ya kuwa angani na abiria wakisafiri kutoka pembe moja ya dunia kwenda ingine? Nani alijua ugonjwa unaweza kusambaa dunia nzima na kutisha wanadamu kiasi hiki? Nani alifahamu kuna siku watu watafungiwa/watajifungia ndani bila kutoka kwa wiki kadhaa? Nani alitarajia hata nchi zinazoitwa Ulimwengu wa Kwanza au nchi zilizoendelea zingepata shida kiasi cha kupoteza maelfu ya raia wake? Ni wakati wa kujifunza na kutafakari tukio la maambukizi ya corona kwa dunia linatufundisha nini. Nimetafakari na kujiuliza sana, hivi kama sabuni na maji vinaua virusi vya corona tunaponawa mikono, au tukitumia sanitizer wanakufa, kweli hadi sasa hakuna “sabuni fulani” ya kusukutua au kumeza ili kuwaua wanapofika kooni au kwenye mapafu? Naamini kuwa hili, pamoja na utaalamu wote walionao wanadamu, ipo haja kumuomba Mungu aingilie kati na kutunusuru. Tangu nimezaliwa, na nimesimuliwa na wakubwa zangu, haijawahi kutokea tukio la ugonjwa kama huu. Kama lipo tukumbushane. Tusikilize ushauri wa wataalamu wa afya, tusafishe mikono. Tusishike midomo, pua au macho. Tuvae barakoa, tuepuke misongamano, tukae nyumbani kama hatuna ulazima wa kutoka. Tupunguze safari zisizo za lazima. Tule vyakula vyenye afya na virutubisho muhimu kama matunda nk. Lakini tusali tukiomba na kukesha pia ili Mungu atunusuru na #covid19 #kaanyumbani #vaabarakoa #vaabarakoasafi #nawamikonokwasabuni mara kwa mara na maji yanayotiririka #epukamisongamano tumia #vitaminc #staysafe #stayhomestaysafe #covid19tzrealities https://www.instagram.com/p/B_BrMmanZ_G/?igshid=95ck1j9v4oxh