Likizo ya uzazi kwa wamama wanaojifungua #mtotonjiti ni siku 84 tu kama wanaojifungua watoto kawaida. @dorismollel kupitia @dorismollelfoundation na washirika kadhaa wamezindua kampeni mahusisi kuhusu umuhimu wa kuwaongezea likizo wazazi wa watoto njiti. Watoto hawa hukaa hospitali wakati mwingine hadi miezi miwili Na mama hurudi nyumbani Na hatimae kazini kabla ya mtoto kupata uzito wa kilo moja na nusu. Pamoja na ukweli kwamba siku 84 hazitoshi kwa mama aliyejifungua mtoto wa kawaida, kampeni inapendekeza angalao miezi 6 kwa mama aliyezaa mtoto njiti, mwezi mmoja kwa baba wa mtoto. Shirima la Kazi duniani (ILO) linapendekeza angalao wiki 14 Na waajiri kufikiria kuongeza hadi wiki 18, wakati Shirika la Afya duniani @who linapendekeza wiki 18. Ziko nchi nyingi duniani zinazotoa muda wa kutosha kwa mfanyakazi akijifungua. Wengine hutoa hadi mwaka Mmoja. Umuhimu wa kufikiria kuongeza likizo ya uzazi kwa kinamama wanaojifungua wakiwa wameajiriwa, ni katika kutambua jitihada zao za makusudi za kujenga taifa letu huku pia wakitekeleza jukumu la kijamii la kuzaa watoto ambao ni taifa la kesho. Jukumu la uzazi sio mchezo, kubeba mimba peke yake ni kazi ngumu. Kulea Mtoto tangu unamzaa hadi anakuwa mtu mzima sio jambo la kawaida. Hata wewe unayesoma ujumbe huu unajua. Tumuunge mkono dada @dorismollel katika kampeni hii muhimu hususani kuwaongezea likizo ya uzazi wamama wliojifungua watoto njiti kutoka siku 84 hadi miezi 6 ili kupunguza vifo vya watoto hawa ambao kwa mwaka wanakufa 11,500 nchini mwetu. #ongezalikizoyauzazi #mtotonjiti #mtotowanesi naunga mkono kampeni hii. #borntoosoon #prematurebabies @womenfund_tz @angella_g_bondo @samia_suluhu_hassan #ummymwalimu @ummymwalimu @wizara_afyatz @ate_tanzania @dr.hmwinyi @kassim_m_majaliwa @bunge.tanzania @ortamisemi @katibanasheria_ @patrobasskatambi_ @ccmtanzania @lemutuz_tv @cloudsfm_ @millardayo @ayotv_ @wasafitv @wasafifm @globaltvonline @globalpublishers @tbc_online @tbctaifa @phillipmwihava @iamrubyafrica @irenepaul001 @stara_thomas @mrishompoto @mcgarab @mcluvanda @mc_linah @mcerickmchome @mc_big_chris @mcpilipili (at Dar es Salaam, Tanzania) https://www.instagram.com/p/CXCyObOIxv4/?utm_medium=tumblr








