VYETI FEKI: SAKATA la DAUDI na PAUL Mheshimiwa Rais na mamlaka nyingine mtusaidie kumaliza huu utata. KAMA maneno ya Gwajima ni Kweli basi Paul anatakiwa kuondolewa na kushitakiwa "Mtu anayetumia cheti cha mtu mwingine awe hai au amekufa anatenda kosa la kughushi nyaraka kwa mujibu wa Kifungu cha 371 cha Kanuni ya Adhabu [Sura ya 16 Toleo la 2002] ya sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na adhabu yake ni kifungo cha miaka saba (7) jela bila faini kwa mujibu wa kifungu cha 337 cha sheria iliyotajwa awali." Na hapa anakuwa na kesi zaidi ya moja. Ina maana hata cheti cha kuzaliwa amegushi, itakuwa hata uhamiaji alitoa Taarifa za uongo. 🙆🙆😣🙄 KAMA maneno ya Gwajima ni uongo, pia anatakiwa kushitakiwa.🙄 VYOVYOTE iwavyo lazima mamlaka zitoe tamko tena mapema sana. Hii ni aibu na fedheha kwa mamlaka za uteuzi. Nakumbuka Rais wakati wa kampeni alisema kwenye Serikali yake akituhumiwa mtu tu amepoteza sifa. Hili la Paul. Je siyo TUHUMA? #Ndalichako #WizarayaElimu #TCU #kamandasirro #utumishi #tamisemi

















