UGONJWA WA SURUA ■ Surua ‘’measles’’ ni ugonjwa unaoweza kuambukizwa kwa urahisi sana, na ulikuwa ugonjwa uliowapata watoto wengi sana kabla ya enzi ya chanjo kuanza. ■ Inaweza kuchukua mpaka siku 10 kabla ya dalili kuonekana baada ya kuambukizwa. Mwanzoni mtoto anapatwa na kikohozi kikavu, kuchuruzika makamasi, macho yakuwa mekundu na baadae homa. ■ Baada ya siku 2 – 4, madoadoa mekundu au kahawia hujiokeza usoni na baadae kusambaa miguuni na mwili mzima. Kunaweza kuwepo madoa meupe kwenye sehemu ya ndani ya mashavu. ■ Watoto wengi hupona vizuri tu. Lakini surua inaweza kusababisha maambukizi sikioni na matatizo mengine kama vile homa ya mapafu na kwa mara chache kuvimba ubongo. □ JIFUNZE ZAIDI HAPA( BIO) 👉https://wikielimu.com/ugonjwa-wa-surua/ #wikielimu #afya #surua https://www.instagram.com/p/CN60JmfLYeA/?igshid=1a1p0eetsa7vx











