kujua Anaweza Kuswali Na Damu Inayotoka (Nifasi) Baada Ya Kusafishwa Mimba, Ijapokuwa Hakuzaa na kupata majibu kwa maswali yako yote tembelea fataawa-al-fiqh
SWALI: Assalaamu alaikum warrahmatullahi wabarakatu Swali linamtatiza dada yetu kwa kupewa majibu tofauti,swali lenyewe ni hili: Dada amekuwa mja mzito kwa miezi 3, na mimba hiyo ikawa haina mafanikio yaani ikafika wakati mtoto matumboni hakui tena na ikabidi hiyo mimba itolewe. Baada ya dada yetu kusafishwa ikawa damu inatoka kama kawaida ya mwanamke akisha zaa. Jee anaweza kuswali na hiyo damu ijapokuwa hakuzaa? Jazaakumullahu khairan. wassalaamu alaikum warahmatullahi wabarakatu










