Dunia kweli dunia, waja wamebadilika, Macho wameyavumbia, maovu yanotendeka, Wongo wamepalilia, na utu umetoweka, Kweli hakuna mkweli, binadamu ni waongo. ~Utunzi wa Justine Bin Orenge #Mwanagenzi
Dunia kweli dunia, waja wamebadilika,
Macho wameyavumbia, maovu yanotendeka,
Wongo wamepalilia, na utu umetoweka,
Kweli hakuna mkweli, binadamu ni waongo.
Makasisi kanisani, nao hawaaminiki,
Wamehini waumini, kuwafanya mashabiki,
Ushuhuda kanisani, hata hausadikiki,
Kweli hakuna mkweli, binadamu ni waongo.
Mahakama yahukumu, wasiotenda maovu,
Kadhongo kwake hakimu, hubadili mtenda ovu,
Uhalalisha…