CLOUDS YAZINDUA SAFARI ZA DALADALA BUZA Mkuu wa Maudhui Clouds Media Group, @sebamaganga akikata utepe kwa ajili ya kuzindua safari (route) za usafiri wa daladala katika barabara ya Mtaa wa Sigara sokoni, Yombo Buza ambao ulisitishwa kutokana na ubovu wa barabara. Usafiri wa daladala ulisitishwa katika eneo hilo kutokana na magari mengi kuharibika kwa sababu ya ubovu wa barabara. Leo ujio wa Clouds Buza safari hizo zimeanza tena na kwamba Clouds Media Group itaweka jiwe la msingi hivi karibuni kwa ajili ya kuanza ujenzi rasmi wa barabara hiyo. Barabara hiyo inajengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Mtaa na Halmashauri Manispaa ya Temeke #SalutiKwaMeme #SikuYaMeme #BuzaNiMchongo #MemesDay #NikisemaNimesemaNaSifuti https://www.instagram.com/p/CQvIsBvMsaV/?utm_medium=tumblr











