Tarehe 3/6/2020 nilitumiwa baruapepe kutoka kwa rais wa shirika moja kubwa sana huko Swideni akinijulisha kuwa nimependekezwa kuwania tuzo ya kimataifa ya uongozi bora iitwayo Tällberg/Eliasson Global Leadership Prize ya mwaka 2020. Shirika hilo linaitwa Tällberg Organization, na rais huyo anaitwa Alan Stoga. Nilipigwa butwaa, kwa sababu ilikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza kulisikia shirika hilo, na ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kupendekezwa kuwania tuzo kubwa kama hiyo ulimwenguni. Kwa bahati mbaya au nzuri sikushinda tuzo ya mwaka 2020, lakini nilishinda kwa sababu mtu kama mimi niliweza kupendekezwa na shirika kubwa ulimwenguni kutokana na kazi ambayo wengi wanaidharau. Thomas Edson alifeli mara 10,000, kabla ya kugundua taa ya umeme. Mimi ni nani kufeli mara moja tu na nilalamike? - Washindi wa mwaka 2020, miongoni mwa viongozi 2,165 waliopendekezwa ulimwenguni kote, kutoka katika nchi 135, ni hawa wafuatao: Sylvia Earle, mwanasayansi wa bahari; Jared Genser, mwanasheria wa haki za binadamu; na Nithya Ramanathan, injinia na mjasiliamali wa mtandaoni. Kila mmoja aliondoka na kitita cha dola 50,000 za Kimarekani na heshima kubwa duniani ya kushinda Tällberg. Ninawapongeza wote kwa ushindi wenu mkubwa wa kihistoria. Asanteni sana Tällberg Organization, asanteni sana mlionipendekeza, kwa kunipendekeza kuwania tuzo ya Tällberg/Eliasson Global Leadership Prize ya mwaka 2020, kwa sababu ya Nukuu za Nyakati Zetu. Kupendekezwa huko kulinipa faraja na nguvu zaidi ya kutokuwa mwendanguu. Asanteni sana kwa zawadi hii. Maneno yameniishia fikrani. Niwatakie wote kila la heri katika shughuli zenu za kila mwaka za kuwatafuta viongozi bora ulimwenguni. Mungu awabariki sana, ninyi na familia zenu. Enock Maregesi, mwandishi wa Kolonia Santita #tällberg #enockmaregesi #sylviaearle #jaredgenser #nithyaramanathan #prizes https://www.instagram.com/p/CKEALNgHhGa/?igshid=87xr2x1hu33c












