MPELELEZI WA TUME YA DUNIA YA KUDHIBITI MADAWA YA KULEVYA KUTOKA TANZANIA, JOHN "MURPHY" AMBILIKILE ("AMBIE") - John Murphy (mtoto wa mwanajeshi – kwani baba yake Gideon Ambilikile alikuwa luteni kamanda wa JWTZ, na babu yake Ambilikile Makojo alikuwa koplo wa KAR katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia) ni mwanajeshi bora kuliko wote Tanzania. Kama Radia Hosni alivyo kwa Tunisia, John Murphy ni miongoni mwa mashujaa adimu waliowahi kukanyaga ardhi ya Tanzania. Akiwa bado kijana, wa miaka 32, John Murphy ni mpelelezi mashuhuri ulimwenguni – kuliko wote katika bara la Afrika – kachero wa kwanza katika historia ya Tume ya Dunia kukamilisha operesheni ya STKJ peke yake (STKJ ni Shabaha ya Tume ya Kiwango cha Juu) bila msaada wowote, na mshindi wa Tuzo ya Shujaa wa Taifa la Tanzania. Kwa sababu za kiusalama, akiwa nje ya Bodi ya Makamishna ya Tume ya Dunia (WBC) na WODEC-Intelligence, John Murphy hujulikana kama John Ambilikile kukwepa shari na mashabiki hususan wanawake; wanaoweza kuleta misukosuko kuonana ana kwa ana na shujaa wa maisha yao. Mashabiki wachache mno wamebahatika kumtambua; huku wengine, kuanzia Tanzania mpaka sehemu za mbali kabisa kama Australia na India, wakibahatika tu kumsikia katika vyombo mbalimbali vya habari. John Ambilikile alizaliwa tarehe 6/11/1960 Jumapili saa saba usiku, Dar es Salaam, wakati huo Tanganyika – wazazi wake walipohamia huko kwa shughuli mbalimbali za kikazi kutokea Arusha, kaskazini mwa Tanganyika, walikokuwa wakiishi. Akiwa na umri wa miaka kumi John alianza kuonyesha kipaji katika sanaa ya mapigano. Wengi walitabiri angefuata nyayo za baba yake, Luteni Kamanda Gideon Ambilikile, aliyekuwa mchezaji mzuri wa miereka katika miaka ya nyuma. John aliweza kucheza sarakasi na kung’fu vizuri bila hata ya kufundishwa na mtu. Soma zaidi hapa: https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=1428384387185385&id=100000415120038 #bmw #johnmurphyambilikile https://www.instagram.com/p/B7UNenynBa1/?igshid=f3rcm3vdfkxs










