Lumba Utifue Vumbi
Wapo walio na uwezo wa kuamba ila huogopa walumbi na magwiji wa kusema. Shairi hili linazinduaaliye na uwezo kwa kumppa ujasiri.
Hunyamazi kuwa simba, nayo lugha huipambi,Hutungi unavyoyumba, wala kwa tungo hufumbi,Waamua kuwa chemba, na kwa maneno huchimbi,Huambi wala kuimba, lumba kutifua vumbi. Kujifungia kwa chumba, ya kipaji huyakumbi,Isiwe tu wajigamba, pasipo kuja ukumbi,Mkulima ni kwa shamba, hendi kuokota simbi,Huambi wala kuimba, lumba kutifua vumbi. Si kwa umbo uwe mamba, lakini nyama hulambi,Usibakie kutamba,…
View On WordPress












