Weekend iliyoisha Siku ya Jumamosi Washkaji zenu @shilawadu kutoka #CloudsMedia Tulikua Visiwani Zanzibar Mjini Magharibi, Tunashkuru Tulipata muitikio Mkubwa Wa waKina Mama na Watoto wao Pamoja na Ndugu zetu wa Kiume kujitokeza Kwa wingi Ktk Uwanja wa Kariakoo, Siku ya Jumapili tukaalikwa Na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi (Unguja) Mh Ayoub Mohammed Ku host Uzinduzi Wa kampeni ya #MimiNaWewe Ikiwa Ni Maalum Kwa ajili ya kuhamasisha Wakazi wa mji huo Kuchangia Damu, Kupima Virusi vya Ukimwi na kuwachangia watu Wenye Uhitaji Kwa Hali na Mali, Tulifika Eneo la Tukio na Kushiriki kikamilifu, Tukaskiliza Kwa Umakini Hotuba ya Mgeni Rasmi ambae ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu, Hotuba ambayo ilikua na Funzo Kubwa Kwa Vijana na RAia wote, Alishauri Vijana Tuache dharau tuwaheshimu wazee Wetu, kuwabeza Au kuwatukana Au kuwasimanga Au kuwapiga wazee Wetu Sio Sifa Nzuri, Aliomba Vijana kudumisha Amani tuliyoikuta ikitunzwa na wazee Wetu, Upendo utawale, chuki ipotee, Tusiwe Wenye kulalamika Sana juu ya Hali Ngumu ya Maisha Bali Tutazame fursa Za kiuchumi Zilizopo kwenye jamii yetu, za kilimo ufugaji elimu Teknohama n.k Kifupi #Shilawadu Tulijifunza mengi kupitia Hotuba Hii, Tunakushukuru Sana Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa Hotuba ambayo Sisi tunaitambua Kama Chakula Cha Ubongo kwani Ni Funzo Kwa Jamii na daima itabaki kwenye Fikra na Matendo yetu . Pia Tulipata Nafasi ya kuzungumza na Kupiga Picha na Mama Samia Suluhu ilikua Ni moment ambayo hatutokuja kuisahau, kwani Alikubali Kuzungumza na Sisi pamoja Kupiga Picha bila figisu japo lilikua Ni Ombi la ghafla, (Makamu wa Rais Ratiba yake Hupangwa Na Walinzi wake Tangu akiwa hajatoka Ikulu, Kwa hyo Sisi kukubaliwa Sio Kitu Cha Spoti Spoti) Huyu Mama Ana Upendo Sana Sana, Tunamshkuru Sana na Tunampenda Zaidi ya anavyotupenda, Lakini Pia shukran nyingine ziende kwa Ofisi ya Makamu wa Rais (Walinzi wake) Shukrani zimfikie Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh Ayoub Mohammed Viongozi wa Manispaa na Wana Mjini Magharibi Kwa kujitokeza Kwa wingi pale . Photo by #OfisiYaMakamuwaRais . #shilawadu #Shukrani #TunakufunguliaDuniaKuwaUnachotaka