Mwanafunzi Tia Ari
Ulingoni najitoma, ya moyoni nieleze Nisibaki na lalama, kwa kalamu nimalize Asilani sitokoma, na tamaa sikatize Tamaa usiikate, siku njema itafika. ~Utunzi wa Bwana Wamui Paul #Mwanagenzi
Ulingoni najitoma, ya moyoni nieleze Nisibaki na lalama, kwa kalamu nimalize Asilani sitokoma, na tamaa sikatize Tamaa usiikate, siku njema itafika.
Darasani ukifika, makinika ufahamu Rafikizo wakichoka, kuimudu na elimu Tamaa ishawatoka, wakabaki bila hamu Kuvua maji ya kina, kwataka mtaalamu
Na nidhamu udumishe, ni muhimu maishani Daima jibidiishe, usilale darasani Yalopita tuyapishe, tuyalenge…
View On WordPress












