Taifa la Muungano wa Visiwa vya Mangrove Vya Ransium, "The United Mangrove Archipelago of Ransium", lililoko katika Bahari ya Pasifiki, mwaka jana lilininukuu katika mojawapo ya mikutano yake ya kimataifa inayohusu mazingira. Taifa hili, kwa mtazamo wangu, ni taifa lenye mambo ya kushangaza sana! Kwa mfano, hakuna Serikali Kuu. Linaendeshwa na serikali za mitaa, na linaamini katika dini iitwayo "Mangrovism" ambayo ni dini ya misitu. Aidha, katika Jamhuri ya Ransium kuoa wake au waume wengi kumeruhusiwa kikatiba kabisa! Ndoa za jinsia moja zimeruhusiwa pia. Pia mtu anapokufa viungo vyake vyote muhimu lazima vitolewe kwa ajili ya kafara, au kwa ajili ya walio hai wanaovihitaji kwa ajili ya afya zao. Katika taifa hilo watoto hujitunza wenyewe. Yaani, hawatakiwi kupata matunzo kutoka kwa wazazi wao au jamii yao ya Kiransium na wanaruhusiwa hata kufanya kazi za kujikimu kwa ajili ya maisha yao wenyewe. Hakuna michezo ya aina yoyote ile wala hakuna kuvuta sigara au mihadarati, na kafara za binadamu zinaruhusiwa bila kificho kwa sababu za kidini. Katika taifa la Ransium hakuna kompyuta, hakuna intaneti, hakuna magari, hakuna ndege (eropleni), na hakuna pombe ya aina yoyote ile. Nilijisikia furaha sana kunukuliwa na taifa linaloongoza kwa utunzaji wa mazingira duniani, ambalo Umoja wa Mataifa ulilichagua kuwa balozi wake wa misitu toka Machi 20 mwaka 2007. Hili ni taifa ambalo watu wengi duniani hawalijui. Haliko kwenye ramani ya Dunia. Liko katikati ya Bahari ya Pasifiki, likiwa na jumla ya visiwa vikubwa 16 vinavyojitegemea; na kwa mujibu wa NSWIK, http://archive.nswiki.org/index.php?title=Ransium, unaambiwa lina watu zaidi ya bilioni 1.4, zaidi ya China au India au Afrika! - Halafu taifa hilo linahamasishwa na nukuu ya Mtanzania ambaye hata hakuujua uwepo wake! Asante sana Ransium kwa kuninukuu, na kwa kuifanya nukuu yangu kuwa kaulimbiu ya mkutano wenu wa majuma mawili kuhusu misitu ya mikoko mnayoithamini sana. Mungu ibariki Ransium. Mungu wabariki Waransium. Soma zaidi hapa: https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=3948955368461595&id=100000415120038 #ransiumarchipelago #nationstates #wastates #enockmaregesi #mangroveforest #environment https://www.instagram.com/p/CKDSreeHZIs/?igshid=daftixh6qqua











