IJUE DAWA YA KULEVYA YA HEROINI KWA UNDANI ZAIDI. BIASHARA KUU YA PILI YA KOLONIA SANTITA BAADA YA KOKEINI, ILIYOMFANYA PANTHERA TIGRISI AWE TAJIRI WA KUTUPWA KATIKA MIAKA YA 80 Heroini hutokana na mmea wa maua uitwao mbaruti-afyuni, ‘oppium poppy’, jamii ya mimea ya mibaruti (‘poppy’) inayopatikana katika sehemu mbalimbali za dunia hususan katika bara la Asia. Mbaruti-afyuni ni mmea mrefu wenye kirungu kidogo kwa juu kama tunda hivi, lenye maua kidogo kwa juu yake. Tunda hilo ambalo hujulikana kama tumba au jicho la ua au ‘poppy pod’ au ‘bud’ kwa utaalamu zaidi, linapokomaa hupasuka na kutoa maua mazuri mekundu ambayo baadaye hutumika kama mapambo katika nyumba za watu. Licha ya kutumika kama mapambo katika nyumba za watu na katika sherehe mbalimbali za kimila, mbaruti-afyuni hutumika kwa kutengenezea chakula na madawa ya kulevya hali kadhalika; kwa sababu za kiuchumi na kiutabibu. Kabla tunda halijaiva na kupasuka, wakulima – kwa kutumia nyembe maalumu – hulikata kwa kulichanja na kutoa afyuni (au utomvu au kasumba au ‘latex sap’ au ‘opium’) au ‘machozi ya mbaruti’. Ndani ya afyuni (utomvu unaotumika kutengenezea heroini) kuna asilimia 12 ya morfini na kemikali nyingine za kialkaloidi zinazojulikana kitaalamu kama ‘opiates’, kama vile thebaini (‘paramorphine’) na kodini (‘3-methylmorphine’). Morfini hiyo baadaye hushughulikiwa kikemia na kutengeneza heroini na madawa mengine kwa ajili ya sayansi na utabibu. Kwa hiyo afyuni inatengeneza morfini na morfini inatengeneza heroini. Aidha, baada ya kutoa afyuni yote ama kwa mikono au kwa mashine, tunda hupasuliwa na kutoa mbegu nyingi ndogondogo zilizokuwamo ndani. Mbegu hizo zenye mafuta huweza kuliwa kama chakula, au huweza kukamuliwa na kutoa mafuta kwa ajili ya kupikia na kwa ajili ya matumizi mengine. Soma zaidi hapa: https://m.facebook.com/koloniasantita/photos/a.518680894843581/1363386367039692/?type=3 #heroin #thamkrabok #thamkrabokmonastery #bettyfordcenter #oxycodone #oxys https://www.instagram.com/p/BrsSNlHHjZ8/?utm_source=ig_tumblr_share&igshid=8ov7t6u113as





