Picha Yazungumza
Picha yazungumza, jua linapochomoza, Angazo la kuangaza, picha isiyo na toza, Mchoraji umekaza, waichora kwa vioza. ~Utunzi wa Abed Anthony #Mwanagenzi
Picha yazungumza, jua linapochomoza, Angazo la kuangaza, picha isiyo na toza, Mchoraji umekaza, waichora kwa vioza.
Macho yao kuyakaza, akili kugugumiza, Kesho wataiunguza, wengine kutoiuza, Mchoraji umekaza, waichora kwa vioza.
Jana yake ilikoza, sababu leo kupoza, Picha moja ya pwaguza, picha akili panguza, Mchoraji umekaza, waichora kwa vioza.
Abed Anthony (Shimbolyo)
View On WordPress















