Urafiki wa kweli ni bidhaa adimu katika nyakati za leo, kwa sababu ya unafiki uliokithiri. Urafiki wa kweli hauangalii faida au hasara ya urafiki wenyewe. Rafiki anayemtumia rafiki yake kwa faida tu bila hasara si rafiki wa kweli. Rafiki wa kweli ni yule anayekuja kwako wakati wengine wote wamekukimbia. Si kila mtu unayemjua anaweza kuwa rafiki yako. Urafiki wa kweli hutegemeana na muda, uaminifu, upendo na kujitoa mhanga kwa ajili ya urafiki. Urafiki wa kweli ni ule ambao rafiki yuko tayari hata kufa kwa ajili ya rafiki yake; kama ilivyokuwa kwa Daudi na Yonathani, mtoto wa mfalme Sauli, katika 1 Samweli 20:25-42. - -Enock Maregesi, mwandishi wa Kolonia Santita #urafikiwakweli #truefriendship #unafiki #hypocrisy https://www.instagram.com/p/BvBZOCJnbZ2/?utm_source=ig_tumblr_share&igshid=1rmvqox6pgclr















