UTUNZAJI SALAMA WA CHAKULA Andaa chakula kwa usafi 1. Safisha vyombo vya kuandalia na kupakulia chakula kwa sabuni na suuza kwa maji safi yanayotiririka. 2. Nawa mikono kabla ya kuandaa chakula. Funika vidonda na michubuko katika mikono yako kabla ya kushika au kuandaa chakula. 3.Tumia maji safi yaliyochemshwa au kutibiwa kwa kusafishia matunda au mboga mboga zinazoliwa mbichi. Tumia mbao au sehemu tofauti za kukatia nyama mbichi/samaki wabichi na kwa kukatia matunda au mbogamboga. 4. Pika vyakula vibichi kwa muda mrefu mfano nyama, kuku, mayai, samaki na vyakula vingine vya baharini. Kwa nyama na kuku, hakikisha supu ina rangi nyeupe na siyo ya pinki. Acha mchuzi na supu vichemke vizuri. 5. Pasha moto viporo mpaka viwe na moto ambao huwezi kugusa. Koroga wakati unapasha moto. JIFUNZE ZAIDI HAPA https://wikielimu.com/utunzaji-salama-wa-chakula/ @wikielimu #hwi_tanzania #wikielimu https://www.instagram.com/p/Cgd4KPFK95H/?igshid=NGJjMDIxMWI=












