Katika jarida la wanyama liitwalo "Voice for Animals" la York, Maine, nchini Marekani, katika toleo lake la Aprili la mwaka 2015, nilitajwa katika ukurasa wa 5 pamoja na paka wawili wazuri wajulikanao kama Jasmine na Niles (ajulikanaye pia kama Niles Wadsworth Longfellow). Hapo tulinukuliwa waandishi wanne: Karen Davidson, Elizabeth Parker, Charles Dickens, na mimi Enock Maregesi. Asanteni sana "Voice for Animals" kwa zawadi, ya kunitambua katika jarida lenu hili la mwaka 2015! Mimi pia ni mpenzi sana wa wanyama. Ndiyo maana mwaka 2009 niliitunga nukuu hii, kwa minajili ya kuwatetea wanyama wote kote ulimwenguni. Nukuu hii imehamasishwa zaidi na mashirika mengi yanayowatetea wanyama ulimwenguni kote. Huwa inanipa faraja sana ninapoona watu kama nyie mkiitumia, tena kwa usahihi! Nawatakia wote heri na fanaka katika shughuli zenu zote za kuwatetea wanyama. Enock Maregesi, mwandishi wa Kolonia Santita #voiceforanimals #enockmaregesi #karendavidson #elizabethparker #charlesdickens #animal #animalsofinstagram #animals https://www.instagram.com/p/CJ8y4MaJleR/?igshid=1l1hhzab08rzm











