NAKULA NA MACHO
Vijana mnao tamba, mlo na nguvu mwilini, Muda wenu kujigamba, upo ni leo jamani, Leo yenu ina bamba, kesho yenu ni usoni, Leo nakula kwa macho, wenye nguvu sikieni.
Nawapigiya kayamba, kwa sauti wastani, Mwenzenu naimba imba, nikiwa huku pembeni, Na leo sina Kilemba, wala mambo hamsini, Leo nakula kwa macho, wenye nguvu sikieni.
Mwili wangu kama mamba, makunyanzi ya mwilini, Kitambo siku za rumba, hungenitowa dansini, Na hata kuruka kamba, nilikuwa namba wani, Leo nakula kwa macho, wenye nguvu sikieni.
Nakumbuka huko pemba, tulikaa baharini, Hatungevaa…
View On WordPress









