Asante kwa maoni yako #Santy_Kimaro kuhusu makala ya Upendo wa Mama kama aliyoandika #Malisa_GJ #TAFAKARI ⬇ Upendo unaozidi wa mama ni wa Mungu tu. Bwana Yesu alikuwa radhi kuacha enzi na mamlaka akaja huku duniani ili awaokoe wenye dhambi ambao wa kwanza wao ni mimi. There is no greater love. Bwana Yesu hataki mwanadamu awaye yote aende kwenye moto wa milele kwani moto ule ameandaliwa Shetani na majini ambayo ni watenda kazi wake. (Mathayo 25:41). 👇 By Malisa GJ, UPENDO WA MAMA Picha hii ilipigwa mwaka 2013 katika mbuga ya wanyama ya Maasai Mara, nchini Kenya na mpiga picha za wanyama (Wildlife photographer) Alison Buttigieg, na kushinda kuwa picha bora ya mwaka katika tuzo za habari huko Australia. Paa/Swala huyu anayesulubiwa na chui hawa, ni mama wa watoto wawili. Akiwa na wanae kwenye maskani yao, walivamiwa na chui waliokua wanatafuta kitoweo. Watoto wake walikuwa wadogo na hawakua na nguvu za kuweza kukimbia na kujiokoa. Mama yao angeweza kuamua kukimbia na kuwaacha wanae ambao wangekuwa vitoweo vya chui. Lakini hakuwaacha. Alikimbia nao. Baada ya umbali kidogo akaona chui wamewakaribia. Akawaacha wanae waende na yeye akapunguza mwendo. Alitaka kuhakikisha wanae wanakua salama hata kama yeye atadhurika. Chui wakamfikia na kumparamia. Katikati ya chui wawili bado aliweza kusimama wima na kuwatizama wanae ambao walikua wakizidi kuyoyoma porini. Alikua akiwatizama kwa mara ya mwisho maana alijua hatawaona tena. Ilikua ni ishara ya kuwaaga. Licha ya maumivu makali ya makucha na meno ya chui lakini hakutizama kando, macho yake yalitizama mbele kuona wanae wanakuwa salama mbali na upeo wa adui. Alijua atakufa lakini hakusikitika maana alijua kifo chake kitaokoa maisha ya watoto wake. Kwa macho yenye ujasiri aliwaaga wanae. Aliwakodolea macho hadi wakapotelea kabisa porini kabla ya kukubali chui kumgeuza kitoweo. Alihakikisha kitu cha mwisho kuona kwenye macho yake ni taswira ya wanae. Ilikuwa ni ishara ya kuwaaga. Alijua hatawaona tena, lakini hakusikitika maana aua kifo chake kilikua ukombozi kwa wanae. #FUNZO: Picha hii inatoa tafsiri halisi ya upendo wa mama. 👇 #FUNZO Inaendelea ukurasa wa maoni















