Ili kuzungumza jambo lolote, tafakari kwanza, pima faida au madhara ya kuzungumza jambo linalohusu heshima yako binafsi, ya taasisi au jamii itakayopokea ujumbe. Chagua wakati muafaka kulizungumza jambo hilo, utazungumza na nani, lini na wapi. Je majira ya kuzungumzia suala husika ni mzuri? Hakuna kingine kinachoweza kuathiri matokeo ya unachozungumzia? Chagua maneno wakati unazungumza. Punguza lugha ya ukali, zungumza kwa heshima, fanya tathmini nini matokeo ya unachozungumza kwa hadhira yako. Kubwa zaidi, unataka wanaokusikiliza wafanye nini? Kwa nini wafanye hivyo? Andaa mpango mbadala endapo ujumbe wako hautafanikiwa kupata matokeo uliyokusudia. Shirikisha wadau muhimu wa ujumbe wako ili ujue nani mtetezi wako au mpinzani wako atakupa sapoti au ataupinga ujumbe wako. Usizungumze jambo gumu wakati una hasira au hisia kali kuhusu unachotaka kuzungumza. Sio wote unaodhani watakuunga mkono watafanya hivyo, kwani watapima umesema nini, Uko sahihi au umekosea. Kumbuka ukishasema jambo, halifutiki kwa kuomba radhi! Linakuwa tayari kwenye “public domains”! #mediatraining #publicspeaking #semantics #meaningofwords #tafakari #kaulinjemanisadaka🙏🙏 @millardayo @wasafi_.media @wasafifm @wasafitv @cloudsfmtz @cloudstv @jahazicloudsfm @tbc_online @azamsports2 #wasafimedia #cloudsdigitalupdates #kondegang # https://www.instagram.com/p/CRprxIzMxwk/?utm_medium=tumblr

















