KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Jibu: Katika jalada la mbele la kitabu cha 'Kolonia Santita' kuna maneno 12 na herufi 82 na nafasi 8 miongoni mwa hayo maneno 12. Kuna jumla ya herufi 90 pamoja na nafasi. Ukiziba myanya yote ya picha kuu ya 'biohazard' ya kitabu utapata namba 88. Sasa tufanye hisabati kidogo: Ukichukua jumla ya herufi (90) gawanya kwa jumla ya maneno (12) utapata 7.5 (Yaani, 90 ÷ 12 = 7.5). 7.5 hapa ni kiashirio ('symbolic'). Na nukta (.) katika elimu ya hisabati ni sawa na alama ya kuzidisha. Msimbo wote wa Kolonia Santita (35 - 12 - 4 - 2 - 88) unatokana na kiashirio hiki cha 7.5! Kwa kutumia kanuni ya kawaida ya sayansi ya namba, MAGAZIJUTO, bila mpangilio maalumu: 7 x 5 = 35 7 + 5 = 12 7 ÷ 5 = 1.4 (1 x 4) = 4 7 – 5 = 2 Ukijumlisha namba zote za msimbo utapata namba 53 (yaani, 35 + 12 + 4 + 2 = 53) ambayo ni kinyume cha namba ya kwanza ya msimbo ambayo ni namba 35. Kwa kuwa jumla ya namba za msimbo ina uhusiano mkubwa na namba ya kwanza ya msimbo, ukizijumlisha utapata namba 88 (yaani, 53 + 35 = 88). 88 hapa inalingana ('corresponds') na 88 ya picha ya kitabu ya tahadhari ya kibiolojia iitwayo 'biohazard'. 88 inawakilisha maneno yote ya jalada la mbele la kitabu cha 'Kolonia Santita'. Hivyo, hizi namba za msimbo zina uhusiano gani na muktadha wa kitabu kizima cha 'Kolonia Santita'? Kumbuka, kuna Kolonia Santita US (Amerika) na kuna Kolonia Santita EA (Afrika Mashariki). Hapa tunazungumzia Kolonia Santita US 35 – Inawakilisha umri wa Frederik Mogens (kachero wa Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya kutoka Denmaki) na imedhihirishwa katika ukurasa wa 113 wa 'Kolonia Santita'. 12 – Inawakilisha umri wa Kikosi Maalumu cha Kikomandoo cha Tume ya Dunia cha Executive Action Corps (EAC). EAC ilianzishwa mwaka 1980 huko Oslo, Norwe. Imedhihirishwa katika ukurasa wa 12 wa 'Kolonia Santita'. 4 – Inawakilisha Vijana wa Tume (makachero wanne wa EAC). Imedhihirishwa katika faslu ya pili ya sura ya kwanza ya 'Kolonia Santita'. Soma zaidi: https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=2287481374609011&id=100000415120038 #msimbo #riddle #koloniasantita https://www.instagram.com/p/BsYXSqKnHCq/?utm_source=ig_tumblr_share&igshid=1biaia3xvzdsq














