Picha hii ni kwa hisani ya Muungano wa Visiwa vya Mangrove vya Ransium, katika Bahari ya Pasifiki, unaoendeshwa na serikali za mitaa, unaoamini katika dini ya Mangrovism. Taifa la Ransium ni taifa la ajabu sana: Kuoa wake au waume wengi kumeruhusiwa; ndoa za jinsia moja zimeruhusiwa; mtu anapokufa viungo vyake vyote muhimu lazima vitolewe kwa ajili ya kafara, au kwa ajili ya waliohai wanaohitaji viungo hivyo. Watoto hujitunza wenyewe, hawatakiwi kupata matunzo kutoka kwa wazazi wao au jamii yao ya Kiransium, na wanaruhusiwa kufanya kazi. Hakuna michezo ya aina yoyote ile. Hakuna kuvuta sigara. Kafara za binadamu zinaruhusiwa kwa sababu za Kimangrovism. Katika taifa la Ransium hakuna kompyuta; hakuna intaneti; hakuna magari; hakuna ndege (eropleni); hakuna pombe ya aina yoyote ile. Raia wa Ransium hawaruhusiwi kuhama nchi. Hakuna serikali kuu. Mamlaka ya kuongoza nchi yako chini ya serikali za mitaa. Kuna kiongozi wa kidini aitwaye Scipio. Kupata taarifa zaidi kuhusiana na taifa hili la Ransium, lenye utajiri mkubwa wa misitu ya mikoko ("mangrove forests"), tembelea mojawapo ya tovuti zake hapa: https://www.nationstates.net/region=forest - -Enock Maregesi, mwandishi wa Kolonia Santita #pasifiki #pacificocean #mangrove #mazingira #environment #scipio https://www.instagram.com/p/BxOwUb2Hqdu/?utm_source=ig_tumblr_share&igshid=tp6xng60u6dc













