Wapo watu ukitaka kuwaua wambie wasome vitabu. Hata ukiwambia someni kitabu fulani kujikinga na kifo wako tayari kufa kuliko kusoma. #vitabu #books #usomaji #reading https://www.instagram.com/p/CAvEx4HHUEv/?igshid=16hh654bphq18
seen from Nicaragua

seen from United Kingdom
seen from China
seen from Nicaragua

seen from Chile
seen from United Kingdom

seen from United Kingdom

seen from United Kingdom
seen from Kuwait
seen from Nicaragua
seen from Yemen

seen from Australia

seen from Australia
seen from Australia

seen from Australia

seen from United Kingdom
seen from United States
seen from Malaysia
seen from China
seen from United States
Wapo watu ukitaka kuwaua wambie wasome vitabu. Hata ukiwambia someni kitabu fulani kujikinga na kifo wako tayari kufa kuliko kusoma. #vitabu #books #usomaji #reading https://www.instagram.com/p/CAvEx4HHUEv/?igshid=16hh654bphq18
MUHTASARI WA UTAFITI WA FALSAFA ZA ENOCK MAREGESI: NUKUU ZA NYAKATI ZETU KATIKA MITANDAO YA KIJAMII. HIZI NI NUKUU ZA NYAKATI ZETU BAADA YA UHURU WA TANGANYIKA MWAKA 1961 Falsafa za Enock Maregesi: Nukuu za Nyakati Zetu zilianza rasmi kufanyiwa utafiti mnamo mwaka 2004, mara tu baada ya mimi kuhamia nchini Uingereza. Tangu mwaka 2004 hadi mwaka 2012 nilifanikiwa kuandika jumla ya nukuu ghafi 516. Oktoba 8, 2012 utafiti ukahamia rasmi kwenye mitandao ya kijamii, kwa ajili ya kupata maoni ya wadau mbalimbali wa nukuu pamoja na falsafa. Kila nukuu kwenye mitandao ya kijamii ilikuwa ikihaririwa na kuhakikiwa tena kwa muda wa juma zima kabla ya kurushwa mitandaoni, kwa ajili ya maoni ya wadau wa nukuu ulimwenguni kote. Kwa hiyo, nukuu ya kwanza iliporushwa Jumatatu ya tarehe 8/10/2012 mitandaoni, nukuu ya pili ilianza kuhaririwa na kuhakikiwa tena hadi Jumatatu ya tarehe 15/10/2012 iliporushwa mitandaoni hali kadhalika. Utaratibu huo uliendelea kila Jumatatu bila kukosa kwa muda wa miaka 7, miezi 3 na siku 12, kuanzia tarehe 8/10/2012 hadi tarehe 20/1/2020. Nukuu 516 zimegeuka kuwa nukuu 365, zilizofanyiwa utafiti kabambe kwa msaada wa wadau mbalimbali wa nukuu ulimwenguni kote, katika mitandao ya kijamii. Nukuu 365 sasa zinahamia kitabuni, zikiwa zimeshafanyiwa utafiti wa kutosha wa zaidi ya miaka 15. Kitabu hiki kitaitwa FALSAFA ZA ENOCK MAREGESI: NUKUU ZA NYAKATI ZETU ambazo ni tofauti na nukuu za wahenga wetu. Falsafa za Enock Maregesi: Nukuu za Nyakati Zetu ni kitabu kilichosheheni jumla ya nukuu 365 za hamasa, kila nukuu na maana au maelezo yake, kila siku na nukuu yake kwa mwaka mzima. Nukuu za Nyakati Zetu zimegusa karibu kila jambo katika maisha ya mwanadamu. Ni kitabu cha maisha chenye vipengele 12 vya maisha ambavyo ni afya, elimu, fedha, furaha, hisia, imani, maadili, mahusiano, tabia, uchapakazi, umoja, pamoja na maisha yenyewe. Zilianza kama Falsafa za Kolonia Santita. Baadaye zikawa Falsafa za Enock Maregesi. Lakini zote ni Nukuu za Nyakati Zetu. Soma zaidi hapa: https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=2985291638161311&id=100000415120038 #nukuuzanyakatizetu #vitabu #books https://www.instagram.com/p/B7h9asXhtBr/?igshid=eeq7rpptgi4g
Kila mwandishi wa riwaya wa kizazi kipya Tanzania anunue angalau kitabu kimoja cha waandishi wenzake na avisome vyote. Bila kusaidiana sisi kwa sisi hakuna atakayetusaidia. Kama mwandishi ameweza kuchapa kitabu cha kwake mwenyewe kwa nguvu kubwa hakika anaweza kununua kitabu cha mwenzake kwa nguvu ndogo. Kila mwandishi wa riwaya wa kizazi kipya Tanzania hana budi kuwa na kampeni ya kusoma vitabu vya wenzake kudumisha uzalendo. Kampeni hii ya usomaji wa vitabu ikianzia kwetu, sisi waandishi, huku tukimweka Mungu mbele, itasambaa hata kwa serikali na kwa Watanzania wote. Badala ya kampeni, utakuwa utamaduni. Sura moja mbaya katika kitabu cha maisha yako haimaanishi kuwa hadithi imeisha. Kampeni yetu ni ya uandishi na usomaji wa vitabu. Kampeni hii kuwa utamaduni lazima tusikate tamaa. Kila mwandishi hana budi kuwa na maktaba ya kwake mwenyewe ya vitabu, kwa ajili ya usomaji na utafiti. Enock Maregesi, mwandishi wa Kolonia Santita #waandishi #authors #vitabu #books https://www.instagram.com/p/B5CIFojHSPT/?igshid=cup3klc2jly9
Wapo watu ukitaka kuwaua wambie wasome vitabu. Hata ukiwambia someni kitabu fulani kujikinga na kifo wako tayari kufa kuliko kusoma. #vitabu #books #kusoma #reading https://www.instagram.com/p/ByAxGBfHunU/?igshid=125ky5w1cojzv
Wakati mwingine katika safari ya kuelekea juu mlimani utajikwaa na kuanguka, utachoka, utakata tamaa, utapata majeraha. Lakini atatokea mtu atakayekwambia simama, kata tamaa kukata tamaa, usiyajali majeraha yako, bali jali mwisho wa safari yako ambapo ni kileleni. Mtu wa namna hiyo haji katika maisha yako kwa kubahatisha. Anateuliwa na Mungu ili akusaidie kufika kwenye "destiny" ya maisha yako, hivyo huna budi kumshukuru na kumtukuza. Kitabu cha MAYA: RAFIKI WA JUANI NA KIVULINI ni kitabu cha kwanza cha M. D. Bwahama kinachomhusu Maya, rafiki yake wa kweli. Kinahusu urafiki adimu kutokea, hasa katika nyakati hizi zenye ubinafsi uliokithiri, wenye faida na mafunzo makubwa kwa jamii zetu. Kinatuonesha jinsi rafiki wa juani alivyo, na jinsi rafiki wa kivulini alivyo. Rafiki wa juani ni rafiki wa wakati wa shida, wakati rafiki wa kivulini ni rafiki wa wakati wa raha. Kitabu hiki kinamwonesha Maya kama rafiki wa juani, na kinamwonesha Maya kama rafiki wa kivulini pia. Pata nakala yako kutoka kwa M. D. Bwahama, 0713-424-802, kwa bei ya kutupa kabisa ya shilingi 3,000 tu! - Kitabu hiki hakina kosa hata moja la kisarufi! Kama lipo, basi ni moja au mawili. Hongera sana M. D. Bwahama kwa mchango huu. Ninakipendekeza kwa kila msomaji, kwa kila mtu. - -Enock Maregesi, mwandishi wa Kolonia Santita #rafiki #bestfriendship #bestfriend #bestfriends❤ #vitabu #books https://www.instagram.com/p/Bv06XlJnv3j/?utm_source=ig_tumblr_share&igshid=9u56azo77e
Kusoma ni kuelewa usiposoma kwa makini hutaelewa. Kusoma ni kuelewa si ukasuku. Kusoma kitabu kama kasuku anavyoimba utaendelea kuimba hutaelewa kitu. Kusoma ni jitihada, si adhabu, lakini ni adhabu ukinyimwa kusoma. Kusoma ni njia mojawapo ya kujipatia maarifa na sioni kwa nini mtu asifurahie kusoma. Soma kwa makini kupata ujumbe uliokusudiwa na mwandishi au waandishi. #kusoma #reading #vitabu #books #bookstagram https://www.instagram.com/p/BqzaU8JnmGD/?utm_source=ig_tumblr_share&igshid=nb7k6kg43bj2
Tiba Yakinifu
Tiba ilo yakinifu, inayoondoa ujinga, Inayotoa uchafu, na akili kuiganga, Hoja zikae kwa safu, kichwani zikijipanga, Maarifa vitabuni, huzitibu zetu bongo. ~Utunzi wa Kinyafu Marcos #Mwanagenzi
Tiba ilo yakinifu, inayoondoa ujinga, Inayotoa uchafu, na akili kuiganga, Hoja zikae kwa safu, kichwani zikijipanga, Maarifa vitabuni, huzitibu zetu bongo.
Huzitibu zetu bongo, watu wakwite kipanga, Ukayapange malengo, vipi uweze jijenga, Ikunuoe kama nyengo, usiwe ja butu panga, Chakula chake ubongo, chatolewa kitabuni.
Chatolewa kitabuni, chakupa afya hakika, Chakutoa taabani, adha isije…
View On WordPress
Taaluma ya Ushairi
Kitabu kilicho chema, hakika nimekisoma, Kila ninapokisoma, unatulia mtima, Nacho ni cha taaluma, ya ushairi nasema, Hongera Bwana Kitula, kwa hichi kitabu chema. ~Ushairi wa Stephen Muia #Mwanagenzi
Kitabu kilicho chema, hakika nimekisoma, Kila ninapokisoma, unatulia mtima, Nacho ni cha taaluma, ya ushairi nasema, Hongera Bwana Kitula, kwa hichi kitabu chema.
Kila ninapokisoma, chanifunza mambo mema, Ushairi ulo mwema, chanifunza nikisoma, Chanipa pia hekima, kukisoma sitakoma, hongera bwana Amata, kwa hichi kitabu chema.
Wanafunzi mnasoma, someni vitabu vyema, Hasa hii taaluma, yawafaa…
View On WordPress