Wapo watu ukitaka kuwaua wambie wasome vitabu. Hata ukiwambia someni kitabu fulani kujikinga na kifo wako tayari kufa kuliko kusoma. #vitabu #books #kusoma #reading https://www.instagram.com/p/ByAxGBfHunU/?igshid=125ky5w1cojzv

seen from Malaysia
seen from United Kingdom
seen from United States

seen from Russia

seen from Malaysia

seen from Russia

seen from Russia
seen from Kuwait

seen from Malaysia
seen from Yemen

seen from Indonesia
seen from United Kingdom
seen from United States
seen from United States
seen from Türkiye

seen from Russia

seen from Indonesia

seen from Maldives
seen from Yemen

seen from Singapore
Wapo watu ukitaka kuwaua wambie wasome vitabu. Hata ukiwambia someni kitabu fulani kujikinga na kifo wako tayari kufa kuliko kusoma. #vitabu #books #kusoma #reading https://www.instagram.com/p/ByAxGBfHunU/?igshid=125ky5w1cojzv
Kuandika hadithi ni kitu kimoja. Kuweka kanuni za fasihi katika hadithi ni kitu kingine. Msomaji wa kawaida wa hadithi au maandiko yoyote hajali iwapo anachokisoma kimeandikwa kwa utaalamu au la – hakuna atakayejali iwapo kanuni za fasihi zitavunjwa ili kupendezesha hadithi au maandiko yoyote. Wengi wanachojali ni utamu wa hadithi wanayoisoma, si kanuni za fasihi zilizotumika katika maandalizi ya hadithi hiyo. Lakini hayo yanaweza kusamehewa. Kisichoweza kusamehewa ni tahajia, sarufi au matumizi ya mazungumzo ya kawaida ya mtaani katika maandiko ya hadithi. Hupaswi kuandika mambo ya kihuni au utani katika hadithi itakayosomwa na watu wengi, kwani wengine hawapendi utani au uhuni hasa wale waliotoa pesa zao kununua hadithi wakitarajia kupata la maana, isipokuwa katika hadithi za vichekesho peke yake. Katika hadithi za vichekesho peke yake ndiyo unaweza kuandika chochote unachojisikia kuandika. Andika mambo ya kihuni au utani ndani ya funga na fungua semi ionekane si wewe uliyesema bali wahusika wako katika hadithi. Usiangalie tu nani atasoma hadithi yako leo, bali angalia nani atasoma hadithi yako miaka mia moja ijayo; na kumbuka, huwezi kumdanganya msomaji. Usiandike kosa kwa makusudi ukidhani msomaji hatagundua. Anaweza kugundua, na akigundua anaweza asiwe shabiki yako tena katika hadithi zako zitakazofuata. Kanuni maarufu katika fasihi ni “Onesha, usiambie”. Ukisema “John alikuwa na furaha,” unamtaarifu msomaji kwamba John alikuwa na furaha. Lakini ukisema “John alitabasamu,” unampa msomaji akili itakayofanya ajue kama John alikuwa na furaha. Unamwonesha, humwambii! Kanuni hii ni nzuri katika fasihi na ndivyo mambo yalivyo katika maisha ya kila siku. Kama John ni mfanyakazi mwenzako, hatuna mtu wa kutuambia kama John ana furaha kwa sababu ya kupandishwa cheo au mshahara. Tunachotakiwa kufanya ni kuchunguza vizuri tabia ya John na kujua nini kinaendelea katika maisha yake. Kuonesha humfanya msomaji azame katika hadithi – hufanya hadithi ionekane ya kweli – hasa mwandishi anapounganisha vyema ubunifu na uhalisia. Soma zaidi: https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=1387146704642487&id=100000415120038 #kuandika #writing #kusoma #reading https://www.instagram.com/p/Bq4mkMiHieF/?utm_source=ig_tumblr_share&igshid=6t1xzuttzrqi
Kusoma ni kuelewa usiposoma kwa makini hutaelewa. Kusoma ni kuelewa si ukasuku. Kusoma kitabu kama kasuku anavyoimba utaendelea kuimba hutaelewa kitu. Kusoma ni jitihada, si adhabu, lakini ni adhabu ukinyimwa kusoma. Kusoma ni njia mojawapo ya kujipatia maarifa na sioni kwa nini mtu asifurahie kusoma. Soma kwa makini kupata ujumbe uliokusudiwa na mwandishi au waandishi. #kusoma #reading #vitabu #books #bookstagram https://www.instagram.com/p/BqzaU8JnmGD/?utm_source=ig_tumblr_share&igshid=nb7k6kg43bj2