Mpatie Mamangu Amani
Mwanawe fasiti boni,sina furaha moyoni, Niyaonayo jamani,hayanipi mi amani, Sijui kakosa nini,humuhumu duniani, Mamangu adhulumiwa,nanyi babu mwangalia, ~Utunzi wa Hosea Namachanja #Mwanagenzi
Mwanawe fasiti boni,sina furaha moyoni, Niyaonayo jamani,hayanipi mi amani, Sijui kakosa nini,humuhumu duniani, Mamangu adhulumiwa,nanyi babu mwangalia,
Hana kweli pa kulima, baba shamba kakodesha, Huu kweli siyo wema,bali yanihuzunisha, Nikijaribu kusema,inanipanda puresha, Zindukeni jomba zangu,mumwokoe mama yangu,
Acheni kuangalia,mamangu akiteseka, Hana furaha kwa ndoa, nisikizeni hakika, Yale…
View On WordPress










