Fuvu la Zinjanthropus liligunduliwa na Mary na mumewe Louis Leakey nchini Tanzania katika Bonde la Oldupai (au "Olduvai Gorge") mnamo mwaka 1959, Julai 17. Fuvu hilo lina umri wa miaka milioni 1.75 kulingana na wanaakiolojia. Lakini Adamu, anayesemekana kuwa mtu wa kwanza kuwapo duniani, aliumbwa na Mungu miaka 6,000 iliyopita kulingana na Maandiko. Je, kati ya Adamu na Zinjanthropus nani hasa aliyekuwapo kwanza kabla ya mwingine hapa duniani? Na je, kama Adamu alikuwa mtu wa kwanza kweli kuumbwa na Mwenyezi Mungu, Zinjanthropus alikuwa ni wa ngapi kuumbwa? #zinjantropus #olduvaigorge #mtuwakwanza #firstman #tanzania🇹🇿 https://www.instagram.com/p/CAKEYaTj112/?igshid=1wa9cu9b42e2p


