Usijiweke kwa mtu, jikite kwenye taasisi. Tumikia taasisi, changia mafanikio ya taasisi, sio mtu. Jenga taswira njema kwa taasisi, usijijengee taswira yako binafsi kama umeajiriwa. Linda maslahi ya taasisi, sio yako binafsi, labda tu kama taswira yako ina tatizo. Linda maslahi ya taasisi, utakuwa umelinda maslahi yako. Usijisemee wewe, semea taasisi yako. Pamoja na malengo yako, kumbuka uko hapo kwa malengo ya taasisi, Ndio maana umepewa hiyo nafasi. Kila kazi Ina mwisho wako. Tabia yako Na matendo yako ndio yatakupa kazi ingine. Kumbuka, watu huajiriwa kwa weledi Na by Eti Vuai ya kuonesha umahiri wa kazi. Wakifukuzwa, hawafukuzwi kwa sababu weledi au vyeti havina tena thamani! Unafukuzwa kutokana na tabia (attitude) zako! Tii viongozi wako, sikiliza ushauri wao. Kiongozi ana mamlaka na sheria pamoja na kanuni za kazi. Zifuate kwa nidhamu, la huwezi, acha kazi hiyo. Ukikisolewa au kuadhibiwa, fuata taratibu. Unyenyekevu Na utulivu ni siri ya mafanikio yako na heshima yako. Hata ukionewa, usipambane, tulia, ukweli siku zote unatabia ya kujidhihirisha. Unaweza usikubaliane Na mimi, inaruhusiwa kukubaliana kutokukubaliana. #carrieradvice #strategicthinking #pr #uhusiano #mahusiano #millardayoupdates #wasafimedia #cloudsdigitalupdates #tbconline @millardayo @cloudsfmtz #mediatraining https://www.instagram.com/p/CRpwhLnss07/?utm_medium=tumblr










