Ishi Kama Mti! Marehemu Mama yangu aliwahi kunieleza kuhusu maisha ya binadamu kuwa kama mti. Tabia za mti kwa wakati wote wa maisha yake, matukio ya misimu mbalimbali, unabaki kuwa mti, miaka na miaka hadi ukatwe au uanguke kwa dhoruba kali. Hata ikija tufani, kabla mti haujaanguka, huinama kwanza na huanguka kwa shida! Sio kirahisi au kwa haraka. Pamoja na uimara wa mti, kuna faida nyingi kutoka kwenye mti. Nikijiandaa kusheherekea miaka 55 ya maisha yangu duniani, natafakari! Hivi nimekuwa mti wa aina gani kwa watu, familia, ndugu, jamaa na marafiki? Kuna miti ya matunda mbalimbali, miti kwa ajili ya kivuli, mapambo Na hata miti kwa ajili ya mbao! Na hata mbao, huweza kutumika kama jeneza, kujenga meli, au hata mlango. Binadamu nao wako wa aina mbalimbali! Kama mti, wako wenye matunda na wako wenye kuwapa kivuli wengine na wako wenye talanta zitakazotumika tofauti na watu tofauti. Nilitamani sana nikiwa mkubwa niwe mti kwa ajili ya matunda, kivuli na baadae mbao. Ikifika wakati wa kuwa mbao basi ama niwe sehemu ya meli kubwa, au mlango mkubwa mzuri! Naamini nimejitahidi kuwa mti mzuri kwa maisha yangu ya miaka 55. Wako watakaoona mti mimi tofauti na wengine! Wako waliokula matunda, waliopata kivuli na wengine hawataona chochote. Napokaribia kuwa mbao wako wanaoona nafaa kuwa mbao kwa kazi mbalimbali. #mtotowanesi #happybirthdaythoughts #miaka55 #millardayoupdates @millardayo # https://www.instagram.com/p/CSI5w84CA18/?utm_medium=tumblr