DIRA YA NUKUU ZA NYAKATI ZETU MTANDAONI TANGU MWAKA 2012 HADI MWAKA 2020 Nukuu za Nyakati Zetu zilianza tarehe 08/10/2012 hadi 08/07/2013, kila Jumatatu, kama awamu ya kwanza ya Falsafa za Kolonia Santita mtandaoni. Awamu ya kwanza ilichukua muda wa miezi 9, au majuma 39, kukamilika mtandaoni. Kuanzia tarehe 08/07/2013 hadi 08/01/2014 kitendawili cha Kolonia Santita, kiitwacho KKS, kilirushwa katika mitandao yote ya kijamii niliyojisajili. Mitandao hiyo ni Facebook, Blogger, Twitter, Bebo, LinkedIn, Scribd, Pinterest, Tumblr, Reddit, na WordPress. Kitendawili hiki kilichukua muda wa miezi 6 au majuma 26 kabla ya jawabu lake kutolewa. Kuanzia tarehe 15/07/2013 hadi 20/01/2014 awamu ya pili ya Falsafa za Kolonia Santita ilisheheni katika mitandao yote ya kijamii niliyojisajili. Awamu hii ilichukua muda wa miezi 6 na Siku 5, au majuma 27, kukamilika mtandaoni. Lakini kuanzia tarehe 08/10/2012 hadi 17/08/2015 Falsafa za Kolonia Santita, awamu zote mbili, zilifikia kikomo katika mitandao ya kijamii. Nukuu hizi zilichukua jumla ya miaka 2, miezi 10 na siku 20 hadi kukamilika kwake, au majuma 150, au jumla ya nukuu 150 za Kolonia Santita. Baada ya hapo nilikwenda likizo ya majuma 16 hadi tarehe 7/12/2015. Tarehe 14/12/2015 Falsafa za Enock Maregesi zilianza rasmi, kupitia nukuu namba 151. Walakini ndani ya hayo majuma 16 ya likizo, nukuu zake zote 16 ziko ndani ya nukuu namba 150. Yaani, nukuu namba 150 imebeba nukuu nyingine 16 kufidia muda wote niliokuwa likizo ya kujinoa ubongo. Kwa hiyo, hata kama sikurusha nukuu mtandaoni, kati ya hizo 16, bado zilijirusha zenyewe bila watu kuziona kwa msaada wa nukuu namba 150. Nitaelezea vizuri zaidi baadaye. Soma zaidi hapa: https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=2985664411457367&id=100000415120038 #nukuuzanyakatizetu #diryamaisha #lifevision https://www.instagram.com/p/B7igxVHhdvH/?igshid=1xbbzxifm3du0