MAJALIWA ATANGAZA NEEMA HANDENI,KILINDI Wananchi wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga wamehakikishiwa kuboreshewa huduma za afya katika halmashauri zote kwa kujengwa hospitali mpya pia kuboreshwa miundombinu ya hospitali zilizopo kutokana na iliyopo kuzidiwa. Hayo yamesemwa na mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM na waziri mkuu Kasim Majaliwa wakati akiongea na wananchi wa wilaya ya Handeni ,katika ziara yake ya siku moja ya kuwaombea kura wagombea wa chama hicho Rais John Magufuli,wabunge wa Handeni na madiwani. Awali mgombea ubunge Handeni mjini Reuben Kwagilwa alisema hospitali ya mji Handeni haina gari la wagonjwa na bado inazidiwa na wagonjwa. Kadhalika John Sallu mgombea wa Handeni vijijini alisema eneo kuna ujenzi wa hospitali hivyo wanaomba fedha zaidi kwaajili ya kumalizia ujenzi huo. Amesema awali walipokewa shilingi 800 milioni kwaajili ya ujenzi wa vituo vya afya ila bado havitoshelezi kutokana na mazingira ya Handeni vijijini. Comment Like Share #KIMAMYTVUPDATES (at Kimamytvonline) https://www.instagram.com/p/CGHYr1IgkzM/?igshid=xxe822irhf2y