MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA WATANZANIA NA WAINGEREZA ,LONDON Picha na Habari za Freddy Macha Ulikuwa mkutano mfupi uliokusudia kutoa shukrani kwa wafadhili na Watanzania London wanaosaidia nyumbani. Fadhila hupitia Jumuiya ya Waingereza na Watanzania (BTS) na kitengo chake cha TDT = shirika la Mfuko wa Maendeleo Tanzania. BTS ilianzishwa mwaka 1975, na mlezi wake sasa hivi ni Rais mstaafu Ali Mwinyi. BTS ilimkaribisha Makamu wa Rais Mheshimiwa Suluhu Samia, aliyekuja London wiki hii kudhuruia mkutano wa Viongozi wa Jumuiya ya Madola. Kawaida viongozi hutegemewa hotuba ndefu zenye maelezo yanayochosha masikio. Mhe Suluhu alitua chuo kikuu cha lugha za Afrika na Mashariki ya Kati (SOAS) akasalimiana na kupeana mikono na wananchi wa pande zote mbili. Hiyo tu ilitosha kuonesha imani yake kwa wananchi wachapa kazi wa pande hizi mbili. Zaidi;ingia https://www.swahilinawaswahili.blogspot.co.uk #@freddymacha14 #Tanzania🇹🇿🇬🇧#makamuwarais#mhesuluhu#mamasamiasuluhu#Watanzaniauk#Uingereza#ubalozi#DkRoseMigiro#mamamigiro#waswahili#england🇬🇧#embassyoftanzania#freddymacha14#Uk#Mswahili#lifestyleblogger#vlogger#Rachelsiwa🙏















