TANZANIA YAPATA MKOMBOZI WA SANAA YA VIJANA.FASDO YAANZISHA BONGO FASHION STYLE COMPETITION 2015 KUSAIDA KUKUZA SANAA
https://youtu.be/1Q2caB_s6sE
In FASDO we are guided by our mission towards: Promoting and developing children and youth talents in arts and sports, encouraging children and youth to work together and rehabilitating, rescuing and protecting youth from drugs abuse, HIV/AIDS,...
BONGO FASHION STYLE COMPETITION, ni moja tu kati ya miradi mingi iliyoanzishwa na FASDO Tanzania.Lakini kwa leo tunazungumzia Mashindano ya sanaa ya Mitindo.
Bongo Style Competition inalenga kutambua, kutoa tuzo/zawadi na kusapoti wabunifu mitindo vijana na wapiga picha vijana na kuhamasisha vijana kupenda sanaa na tamaduni zao. Bongo Style Competition kwa wabunifu mitindo vijana na wapiga picha vijana ni kwa ajili ya vijana wenye umri wa miaka kati ya 18 hadi 25. Shindano lina vipengere viwili: Mbunifu Mitindo bora kijana na Mpiga picha bora kijana.
Shindano ni kwa vijana wa kitanzania tu wenye umri wa miaka kati ya 18 hadi 25). Vigezo na masharti yafuatayo yatazingatiwa wakati wa tathmini:
Ubunifu, kujieleza, upekee na usafi wa kazi/muonekano wa kazi.
Kazi zote ziongelee tamaduni za kitanzania, urithi/amali na hali halisi ya kitanzania. Iwe inayoweza kuchapishwa (isiwe inayokiuka maadili, isiwe na udhalilishaji wa aina yoyote) na isiwe imewahi kuchapishwa/kutolewa au kushindanishwa kwenye mashindano mengine kabla.
kazi iwe ni ya ubunifu wa mshiriki kwa asilimia 100%.
KUMBUKA: Vigezo na masharti mengine yapo kwenye maelezo ya kila kipengere cha ushindani.
Jinsi/namna ya kushiriki:
Jiandikishe(fomu ya kujiandikisha)
Itume kazi yako (fomu ya kutuma kazi)
kila kazi lazima iwe na kichwa cha habari.
ushiriki wote lazima uzingatie uelewa wa taarifa za vigezo na masharti ya shindano.
Tarehe za Mwisho wa Kushiriki
Tarehe 11 mwezi wa kumi: Mwisho wa kujiandikisha kwenye mtandao
Tarehe 15 mwezi wa kumi: mwisho wa kutuma kazi
Tarehe 20 mwezi wa kumi : Kutangaza 20 bora
Tarehe 4-5 mwezi wa kumi na moja (Mafunzo kwa washiriki 20 bora)
Tarehe 8 mwezi wa kumi na moja – kutangaza kumi bora kwa ajili ya fainali
Tarehe 9 hadi 22 mwezi wa kumi na moja: Upigaji kura kwenye mtandao
Tarehe 27 mwezi wa kumi na moja: Kutangaza washindi
mshindi wa kila kipengere (Mbunifu mitindo na mpiga picha) atajishindia Tsh milioni moja pesa taslimu na safari ya ubelgiji kuonyesha kazi zao). Safari inatarajiwa kuwa mwezi wa tatu mwaka 2016. Washiriki wote waliongia fainali watapatiwa misaada mbalimbali katika kuendeleza vipaji vyao. Msaada huu utakuwa katika kuwatangaza, kuwakuza, na kusaidia umiliki wa kazi zao kisheria.
Royal fashion Tanzania Inawashukuru kwa dhati na inawapongeza FASDO Tanzania kwa kuweza kujituma kwa hali na mali kuhakikishawanawapa Ari na hamasa vijana kufanya kazi na kujituma katika kutumia vipaji Vyao.Lakini pia tunaomba makampuni mbalimbali waweze kuchangia na kusapoti kwa hali na mali miradi hii yenye Tija kwa Taifa letu la Tanzania ,Bara letu la Afrika na Dunia kwa Ujumla.TUNAWATAKIA KILA LA HERI KATIKA MIRADI HII
via Blogger http://ift.tt/1MCznZC