Unapojaza upepo kwenye mpira wa miguu, kwa mfano, kwa kutumia pampu, kisha mtoto akautoboa mpira huo kwa msumari; upepo utarudi kwenye pampu au utapotelea hewani? Upepo utapotelea hewani. Wakati Yesu anapata taarifa ya kifo cha Lazaro, rafiki yake, kama inavyoelezwa katika Yohana 11:11-14, roho ya Lazaro ilikuwa haijaenda popote: si mbinguni wala kuzimu; ndiyo maana Yesu akawambia wafuasi wake kuwa Lazaro alikuwa amelala usingizi. Je, kuna tofauti yoyote kati ya usingizi na kifo? Kama ipo ni ipi? Kifo na usingizi ni mtu na ndugu yake! Lakini kuna tofauti. Usingizi ni hali inayohusiana na mwili, akili na ufahamu; wakati kifo ni hali inayohusiana na mwili, akili, ufahamu na roho! Mtu anapolala usingizi kinachohama ni ufahamu. Anapokufa kinachohama ni akili, ufahamu na roho. Kuna usingizi wa kawaida na usingizi mzito au usingizi wa pono. Usingizi wa pono hauna tofauti sana na kifo, kuliko vile ulivyo usingizi wa kawaida. Kwani ufahamu huwa unachagua ama urudi kwenye mwili na akili au utokomee kabisa katika ulimwengu wa roho, ili uzaliwe upya katika mwili mwingine na akili nyingine. Lakini ufahamu hauwezi kutokomea kabisa katika ulimwengu wa roho kwa mtu aliyelala usingizi wa kawaida au wa pono. Kwa sababu, kabla haujahama unajishikiza kwenye wazo la mwisho la mtu kabla mtu hajapitiwa na usingizi. Kwa hiyo lazima urudi baadaye, isipokuwa pale roho ya aliyelala inapokuwa imehama pia. Mungu alimuumba mwanadamu ambaye ni mkusanyiko wa mwili, roho na maisha. Mtu anapolala ufahamu wake, uliomo ndani ya roho yake, hutoka; hivyo kumfanya awe na sifa fulani za kifo. Yaani, asijue chochote kinachoendelea, asiwe na ufahamu wowote, asiwe yeye kabisa, asiweze kufikiria chochote, asiweze kuona wala kunusa chochote. Kama hivyo ndivyo, je, tunapolala huwa tunakufa kwa muda? Vyovyote jibu litakavyokuwa, tunapaswa kuyaheshimu maisha. - -Enock Maregesi, mwandishi wa Kolonia Santita #usingizi #sleep #maisha #life #kifo #death https://www.instagram.com/p/BwEzE65nExy/?utm_source=ig_tumblr_share&igshid=oxr5xq7x8xjf













