#ushuhudawangu #YesuWewe Huwa ni kawaida yangu kuwahudumia wajawazito na wanaotarajia kujifungua. Siku moja mama mmoja alipokuwa karibu na kujifungua ndani ya saa moja alipiga kelele za kuashiria hatari ya Maisha dhidi yake. "nakufaa!... Nakufaa!!..." Baadae kama dakika moja hivi akakumbuka kuwa Hata yeye alizaliwa na mama yake. Hivyo akaita kwa sauti kuu ya ajabu "Mamaaa...! Mamaa wee!" Lakini kadri hatua ya #utungu (uchungu) wake ikizidi kuwa juu akakumbuka kuwa #YESU ndiye aliyepo upande wake. Akaita kwa sauti ya Unyenyekevu sana "Yesu.... Yesu... Nisaidie mwanao." ......... Katika maisha ya kawaida WANADAMU tumeumbwa kustahimili maumivu kwa namna yetu wenyewe. Maumivu ya kutokuwa na kazi, ajira, biashara, ndoa, elimu, ndugu, watoto, na hata maumivu ya magumu TUNAYOPITIA. Lakini katika hayo yote TUNAYOPITIA yupo msawazishaji ambaye ni YESU. MWENYE KIPIMO CHA KWELI JUU YA MAISHA YETU. unapopatwa na jaribu, mwanzo wa maumivu yake hauwezi kuwa sawa na mwisho wake. Lakini Usiogope pindi unapokuta unamwomba Mungu akuvushe kwenye jaribu hilo na kwa wakati huo huo ukakuta jaribu linaongezeka Ukubwa wake. Ukubwa wa mzigo unapoongezeka jua ya kuwa ndio mwisho wa jaribu unapokaribia. Kumbuka Sio kila hatua ngumu unazozipitia ni za mpango wa shetani. Zingine zimewekwa mbele yako kwa utukufu wa Mungu. Ili ukishinda, Mungu ajitukuze kupitia wewe. Tazama video yangu mpya ya #YesuWewe YouTube. Cc @jaclinemalekela @worshiper_farida @mc_joshua_makondeko @goodluckgozbert @edithamugisha @filiboy255 @ambwenemwasongwe_official @mwana2milongo (at Africa/Dar_es_Salaam)









