Hatari ya Heroin na Madawa mengine ya kulevya... Heroine hustua seli za ubongo kuzalisha homoni aina ya Dopamine ambayo humfanya mtu kusikia raha. Homoni hii hutolewa kwa kiasi cha unit 1200- 1800 baada ya kutumia heroine kulinganisha na unit 150 - 200 tu zitolewazo wakati mtu anaposhiriki ngono. Ndio kusema Heroin inaleta raha karibu mara tisa ya ile itokanayo na ngono, tena kwa muda wa takribani dakika 30-40. Raha hii huitwa kwa kitaalamu Euphoria. Homoni hizi za dopamine hutolewa kwa wingi sana kiasi cha kuufanya mwili kutengeneza vipokezi (receptors) zaidi na zaidi. kwa hiyo mwili hutamani heroin zaidi na zaidi ili kukidhi matakwa ya vipokezi vinavyozalishwa...hali hii huishia kumfanya mtumiaji kuhitaji idadi kubwa zaidi ya heroin (tolerance) Arosto/withdraw symptoms Wakati Heroin inapoisha mwilini, mwili hutamani zaidi. Hapo ndipo hutokea arosto, ambapo mtumiaji hutaabika kwa kukosa raha isiyo kifani. Maumivu makali ya tumbo, viungo na kichwa, baridi kali, mapigo ya moyo kwenda kasi, mwili kutetemeka, kujisikia vibaya sana, kuchoka, kushindwa kula na dalili nyingine mbaya humpata. Hali hiyo humlazimu kwa haraka sana kutafuta namna ya kuipata Heroin iwe kwa njia halali au haramu... Uthithubutu kutumia hizi makituuu.. Afya Yako Ni Bima Bora Zaidi Kwako Anza kujenga Afya yako kwa (at Dar es Salaam, Tanzania)









