MAONO YA MCHUNGAJI MKUU WA KONDOO ZA BWANA MUNGU Mchungaji mwenye akili ni lazima atatendea Kazi maono ya Bwana Yesu, kwa kutafuta na kuchunga kondoo wa zizi hata walioko zizi jingine kwa utukufu kama ilivyoelezwa katika Kitabu cha #YOHANA 10:16: Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja. [AMP] - John 10:16 And I have other sheep [beside these] that are not of this fold. I must bring and impel those also; and they will listen to My voice and heed My call, and so there will be [they will become] one flock under one Shepherd. Kwa msingi huo, kanisa la #Full_Gospel_Bible_Fellowship lina wafuasi maelfu elfu kama nyota za mbinguni, zilizo sambaa katika kona nne za Ulimwengu. Shetani hataki ifahamike kwamba, #bishopzacharykakobe ana wafuasi ndani na nje ya kanisa analoongoza pamoja na Huduma ya #bzkim (Bishop Zachary Kakobe International Ministries) inayotenda kazi ya kuhubiri Injili kwa kila kiumbe ili yamkini mataifa wawe ni wanafunzi wa Yesu kwa kuyashika mafundisho ya Kristo kama yanenavyo maandiko matakatifu kwenye Biblia. Ndugu ! Iwe Jua au Mvua; tumwamini Mungu na mtumishi wake , kwa kuzidi kumtegemeza Baba askofu Zachary Kakobe na familia yake, kinyume na mawazo ya kuzimu na majeshi ya Ibilisi yanayoibuka kila itwapo leo; tunaposubiria parapanda ya kulinyakua kanisa (watakatifu) katika siku hizi za mwisho wa dunia zinapokaribia. https://www.instagram.com/kongwastone/p/Bdm1VT-FXiD/?utm_source=ig_tumblr_share&igshid=1gu9ug0md1nk7













