Chungu na Pegiko
Kutegemea pegiko, ndio tabia ya chungu Kisipate hangaiko, kikaja tenguka tengu Kama mwana na mbeleko, huwezi engua engu Mambo huenda mtengu, chungu pasi na pegiko ~Utunzi wa Hamisi Kissamvu #Mwanagenzi
Kutegemea pegiko, ndio tabia ya chungu Kisipate hangaiko, kikaja tenguka tengu Kama mwana na mbeleko, huwezi engua engu Mambo huenda mtengu, chungu pasi na pegiko
Chungu pasi na pegiko, itakufika mizungu Utapata hangaiko, huwezi kuvuga dengu Adha yake mnenguko, kila muda nengunengu Mambo huenda mtengu, chungu pasi na pegiko
Chungu pasi na pegiko, ni duni usoni mwangu Inanipa hamaniko, mnani watu…
View On WordPress











