Tarehe 20/1/2020 ndiyo mwisho wa utafiti wa Falsafa za Enock Maregesi: Nukuu za Nyakati Zetu katika mitandao ya kijamii. Safari ya miaka 7, miezi 3 na siku 12, au majuma 365, hatimaye itafikia kikomo. Saa 8:00 usiku wa tarehe hiyo, 20/1/2020, itarushwa nukuu ya mwisho namba 365. Saa 2:00 asubuhi utarushwa muhtasari wa utafiti wa Falsafa za Enock Maregesi: Nukuu za Nyakati Zetu katika mitandao ya kijamii, pamoja na mfano wa jalada la kitabu cha Falsafa za Enock Maregesi: Nukuu za Nyakati Zetu. Katika muhtasari huo utajua ni nini kilisababisha kitabu cha maisha kiitwe “Nukuu za Nyakati Zetu”, na pia utajua hizo “Nyakati Zetu” ni kipindi gani hasa; katika vizazi vyetu vya jana, leo na hata kesho. Saa 8:00 mchana itarushwa DIRA YA NUKUU ZA NYAKATI ZETU MTANDAONI TANGU MWAKA 2012 HADI MWAKA 2020, pamoja na kaulimbiu ya kitabu cha Falsafa za Enock Maregesi: Nukuu za Nyakati Zetu. Katika dira hiyo utajua baadhi ya siri zilizojificha ndani ya Nukuu za Nyakati Zetu mtandaoni, kama sehemu ya dira ya maisha yangu, ikiwa ni pamoja na fumbo la nukuu 16 kujificha ndani ya nukuu 1. Kadhalika, utadokezwa (hutapewa jibu) kuhusu fumbo la Shirika la Afya Duniani (WHO). Fumbo hilo limejificha kama picha katikati ya tarehe 17/1/2013 na tarehe 14/9/2015 katika kalenda au makavazi ya akaunti yangu ya tovuti ya WordPress (www.enockmaregesi.wordpress.com). Aidha, utadokezwa kwa nini Nukuu za Nyakati Zetu katika tovuti za Blogger na WordPress zilisitishwa ghafla tarehe 15/6/2018 badala ya tarehe 18/6/2018. Tarehe 18/6/2018 ndiyo iliyokuwa siku yangu ya kawaida ya kurusha nukuu, lakini nikarusha nukuu 8 mfululizo tarehe 15/6/2018. Miaka 7 iliyopita nilihuluku Dira ya Nukuu za Nyakati Zetu Mtandaoni Tangu Mwaka 2012 hadi 2020. Ndoto hiyo ITATIMIA hatimaye, kwa kudura za Mwenyezi Mungu, saa 8:00 usiku wa tarehe 20/1/2020. Enock Maregesi, mwandishi wa Falsafa za Enock Maregesi: Nukuu za Nyakati Zetu #nukuu #quotes #nukuuzanyakatizetu https://www.instagram.com/p/B7P2DcDnGjM/?igshid=13wwtl3dv97sd