
seen from Italy
seen from Ireland
seen from United Kingdom

seen from Italy
seen from Ireland

seen from Poland
seen from Australia
seen from Türkiye
seen from France
seen from United States
seen from Türkiye

seen from France

seen from Japan

seen from Germany
seen from Malaysia

seen from Germany
seen from United States
seen from Chile
seen from United States

seen from Argentina
Sentensi zifuatazo zimekosewa kisarufi: - (A): Historia ya maisha yangu ni yangu. Wewe ni nani kusema historia yangu si ya kweli?? - (B): Malima; hivi ni kweli kuwa mwanao alisema, "Je, kiko wapi kikombe cha chai?"? - Alama ya kuuliza ina kanuni zake katika sarufi, kama ilivyo koma. - Katika fani ya fasihi andishi kuandika alama mbili au zaidi za kuuliza mwishoni mwa swali la moja kwa moja ni kosa, kama ilivyo kosa kuandika alama hata moja tu ya kuuliza mwishoni kwa swali lisilo la moja kwa moja. - Mfano wa swali la moja kwa moja ("direct question") ni: "Je, utanisindikiza katika safari yangu ya Kuba?" huku mfano wa swali lisilo la moja kwa moja ("indirect question") ukiwa: "Nauliza kama utanisindikiza katika safari yangu ya Kuba." - Kwa hiyo, kwenye sentensi zetu za mfano hapo juu, ukiondoa alama moja ya kuuliza katika kila sentensi utapata sentensi sahihi zifuatazo: - "Historia ya maisha yangu ni yangu. Wewe ni nani kusema historia yangu si ya kweli?" - "Malima; hivi ni kweli kuwa mwanao alisema, 'Je, kiko wapi kikombe cha chai?'" - Waandishi wengi hutumia alama nyingi za kuuliza katika sentensi zao, wakati mwingine bila kujua, kwa minajiri ya kuonesha msisitizo wa jambo fulani. Lakini hakuna haja ya kufanya hivyo, kwani kufanya hivyo ni kuonesha utovu wa nidhamu katika lugha. - Kimsingi sentensi ya kwanza hapo juu (A) imekosewa kwa sababu tu ya alama ya kuuliza, na sentensi ya pili (B) imekosewa pia kwa sababu tu ya alama ya kuuliza, ijapokuwa waandishi wengi hulichukuliwa kosa hilo kama kosa dogo tu lisiloweza kugunduliwa na wasomaji. Mtindo huo wa kiuandishi ni uvunjifu wa kanuni ya alama ya kuuliza. - Katika sentensi ya pili (B) yapo maswali mawili ya msingi ndani ya swali moja yanayoulizwa: Yaani, swali linalosemekana kuulizwa na mtoto; pamoja na swali la jumla la yule anayemuuliza Malima kama mtoto aliuliza swali. Katika sentensi hiyo hakuna haja ya kuweka alama ya kuuliza mwishoni mwa swali kuu la jumla; kwani swali alilouliza mtoto linatosha peke yake kuwa na alama ya kuuliza. - Soma zaidi hapa: - https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=2495331523823994&id=100000415120038 - #alamayakuuliza #questionmark #kiswahili #swahili #sarufi #grammar https://www.instagram.com/p/BxuiARCHaUO/?igshid=rwl54h7k9pis
Soma sentensi ifuatayo kwa makini: - "Kiswahili, lugha ya biashara na mawasiliano ya Kenya, Tanzania na Uganda, ni miongoni mwa lugha 100 mtambuka Afrika, na duniani kwa jumla." - Je, sentensi hii imekosewa kisarufi au iko sahihi? #koma #mkato #comma #sarufi #grammer https://www.instagram.com/p/Bxook8cH16H/?igshid=1xtknv2kj3a0p