Bila upinzani wa kweli nchi haiwezi kutawalika, ijapokuwa inaweza kutawaliwa bila upinzani wa kweli. Kutawalika ni kukubali kutawaliwa; kutawaliwa ni kukubali kutawalika. Bila upinzani wa kweli hakuna uzalendo wa kweli; bila uzalendo wa kweli hakuna upinzani wa kweli. Kuwa mpinzani wa kweli wa serikali, kwa kuwa mzalendo wa kweli wa nchi yako; itetee nchi yako kutoka moyoni, katika masuala ya msingi ya katiba ya nchi. Upinzani ni changamoto; na bila changamoto nchi haiwezi kutawalika, ijapokuwa inaweza kutawaliwa kidikteta. Kama nilivyosema hapo awali, kuna tofauti kati ya kutawaliwa na kutawalika. Kutawalika ni kukubali kutawaliwa; na kutawaliwa ni kukubali kutawalika. Serikali ya kidikteta ni serikali inayotawala nchi iliyoshindikana kutawalika; na nchi iliyoshindikana kutawalika ni nchi yenye upinzani wa kweli dhidi ya serikali isiyokubalika kwa wengi. Changamoto hata katika kipindi cha Awamu ya Kwanza cha utawala wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zilikuwapo. Yaani, kwa muktadha wa nukuu hii, upinzani ulikuwapo; ndiyo maana nchi ilitawalika, na ndiyo maana mifarakano ya hapa na pale haikuisha. Kwa hiyo, changamoto ni muhimu katika ustawi au uendeshaji wa nchi yoyote. Mifarakano katika nchi husababishwa na upinzani wa kweli wa ndani au nje ya nchi dhidi ya serikali isiyokubalika. Vivyo hivyo, kutengana katika nchi husababishwa na upinzani wa kweli wa ndani au nje ya nchi dhidi ya serikali isiyokubalika. Bila upinzani wa kweli hakuna nchi itakayotawalika kikatiba, ijapokuwa kuna nchi zinazoweza kutawaliwa kidikteta bila upinzani wa kweli. Mtu anaweza kuuliza, “Mbona nchi za kidikteta zinatawalika pasi na upinzani wowote?” Hapana! Nchi za kidikteta hazitawaliki; bali zinatawaliwa, kidikteta, kwa sababu ya upinzani wa kweli wa ndani au nje ya nchi husika. Soma zaidi hapa: https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=2480580955299051&id=100000415120038 #upinzani #opposition #changamoto #challenges #udikteta #dictatorship #uzalendo #patriotism https://www.instagram.com/p/BxYWhZShMoO/?utm_source=ig_tumblr_share&igshid=1vm1ud3i72gvn













