Wachawi hawamwabudu Shetani kwa sababu dhana ya Shetani ni dhana ya Kikristo, na wachawi si Wakristo. Wachawi hivi ndivyo wanavyoapishwa na kuikana imani ya Kikristo: Mwanafunzi hupelekwa kilingeni katika siku maalumu kuonana na Shetani, pamoja na jopo la wachawi. Shetani hutokea katika mwili wa hewa, mwili uliochanganyikana na hewa na mvuke mzito, wa mwanamume na kuwasihi waishikilie imani yao kwake kwa mioyo yao yote, huku akiwaahidi utajiri na maisha marefu kama hawatamkana. Kisha wachawi wanampendekeza mwanafunzi kwa Shetani. Shetani humuuliza mwanafunzi kama yuko tayari kuikana imani yake, kuachana na Ukristo na kutokumwabudu Mwanamke Aliyebarikiwa Kuliko Wanawake Wote Duniani Bikira Maria, na kutoziheshimu sakaramenti za aina zote. Mwanafunzi atakapokubaliana na masharti hayo, Shetani atanyoosha mkono wake na kumsihi mwanafunzi anyooshe wa kwake pia. Kwa mkono wake mwenyewe, mwanafunzi ataapa na kuweka agano na Shetani mbele ya jopo la wachawi. Baada ya hapo bila kuchelewa Shetani ataendelea na kusema kuwa hicho kiapo hakitoshi. Lakini mwanafunzi atakapouliza afanye kitu gani cha ziada, Shetani atahitaji kiapo kifuatacho kwa heshima yake na kwa heshima ya mashetani wote: Mwanafunzi ajikabidhi kwa Shetani kwa mwili na kwa roho yake yote daima dawamu, na afanye kila awezalo kuleta wanafunzi wengine wa kike na wa kiume katika ufalme wake. Kama hiyo haitoshi Shetani ataongeza kuwa lazima mwanafunzi atengeneze mafuta fulani kutokana na mifupa na viungo vya miili ya watoto, hasa watoto waliobatizwa, kwani kwa kufanya hivyo atamtimizia kila kitu atakachokitaka hapa duniani. Njia nyingine ya kiapo ni kwa wale ambao hawajiamini au wana hofu ya kuonana na Shetani uso kwa uso kilingeni, akiwa na mwili wa kimazingaombwe na sauti ya kutisha kwani Shetani hana mapafu wala hana ulimi. Badala ya kilingeni mwanafunzi hupelekwa kanisani na jopo la wachawi ambapo mbele ya jopo atalazimishwa kuikana imani yake, kumkana Yesu Kristo, kuukana ubatizo na kulikana kanisa zima kwa ujumla wake. Soma zaidi: https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=2291367150887100&id=100000415120038 #wachawi #witches #shetani #satan https://www.instagram.com/p/BsfNsR3nQzO/?utm_source=ig_tumblr_share&igshid=f8cju6ptqxbu














