DHANA POTOFU KUHUSU UKIMWI ■ Ukimwi ni upungufu wa kinga mwilini unaosababishwa na virusi. Virusi hushambulia mwili na kusababisha kinga ya mwili kushuka na mwili kuweza kushambuliwa na magonjwa nyemelezi. ■ Njia kuu ya maambukizi ya ugonjwa huu ni ngono isiyo salama. Hadi sasa, bado hakuna tiba ya ugonjwa wa Ukimwi, lakini kuna dawa zinazotumika kupunguza makali ya ugonjwa huu. ■ Matumizi ya mapema ya dawa za kufubaza virusi ”ARV” yatakuwezesha kuishi ukiwa na afya njema. Ni muhimu kupima afya ili kujitambua na kuchukua hatua mapema. ■ Ingawa maarifa ya ugonjwa huu ni mengi, bado kumeendelea kuwepo na changamoto nyingi katika jamii yetu. Moja ya changamoto hizi ni imani potofu iliyojengeka katika jamii, inayopelekea uoga wa kupima kwa kuhofia unyanyapaa wa waathirika utakaofuata. ■ Hali hii hurudisha nyuma harakati za mapambano dhidi ya ugonjwa huu. □ JIFUNZE ZAIDI KUHUSU DHANA HIZI HAPA [BIO] 👉 https://wikielimu.com/imani-potofu-kuhusiana-na-vvu-ukimwi/ #wikielimu #afya #afyayako #ukimwi https://www.instagram.com/p/CNt6xiZLtTl/?igshid=rsd72zwoy92l













