KUPUNGUZA UZITO NI KUNAHITAJI MPANGO ■ Mtindo wa maisha unaohusisha mazoezi ya mara kwa mara, pamoja na ulaji wa chakula bora ndio njia bora zaidi ya kupunguza uzito. Kupungua kwa uzito, hata kama ni kidogo tu, kunaboresha afya ya mtu. Msaada kutoka kwa familia na marafiki ni muhimu sana. ■ Wakati unapochagua aina ya chakula na muda wa kula, lengo lako kuu linapaswa kuwa kujifunza njia mpya za mtindo wa maisha ili uzifanye kuwa utaratibu wa kila siku wa maisha yako. ■ Watu wengi wanaona vigumu kubadili tabia zao za ulaji. Watu hawa wanahitaji kuhamasishwa kufanya mabadiliko ya mtindo wa maisha.Unapaswa kuyafanya mabadiliko hayo kuwa sehemu ya maisha yako. ■ Kushauriwa na mtaalamu wa chakula na mlo husaidia kuweka malengo safi, bora kiafya na yanayotekelezeka, hii husaidia kupunguza uzito huku ukiendelea kuwa na afya njema. ■ Kujinyima chakula kulikokithiri si salama na mara nyingi hakufanyi kazi vizuri. Kujinyima chakula kulikopitiliza husababisha mtu kula vyakula visivyo na vitamini na madini ya kutosha. Watu wengi wanaojaribu kupunguza uzito kwa namna hii hujikuta wamerudi tena kwenye mtindo wao mbovu wa kula chakula na huongezeka tena uzito maradufu. ■ Watu wengi wanapokuwa na msongo wa mawazo hujikuta wakila chakula kila wakati na hii husababisha wao kuongezeka uzito. Jifunze njia mpya za kudhibiti msongo, badala ya kujifukia kwenye chakula. Kwa mfano, fanya mazoezi, ongea na mtoa huduma ya afya kama una sonona ili akusaidie. □ JIFUNZE ZAIDI HAPA 👉https://wikielimu.com/kitambi/ #wikielimu #uzito #afyayako https://www.instagram.com/p/CNCkqT0rXep/?igshid=jzt2vc3qzt07










