NAWATAKIA HERI YA PASAKA KWA KUWA TUNAKUMBUKA BWANA WETU YESU KRISTO AMEFUFUKA KAMA ALIVYOSEMA; HALELUYA !!! Imetupasa kusherehekea sikukuu ya Pasaka kwa furaha kuu na shangwe tukikumbuka kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo; aliyeshinda mauti kwa Uzima;Haleluya !!! (1WAKORINTHO 15:32-58) Ikiwa Yesu Kristo Mwokozi mkuu wa ulimwengu alishangilia msalabani kwa mikigo kwa ushindi ni zaidi sana Mimi na wewe kusherekea pasaka kwa kusambaza Ujumbe maalum wa msalabani kwa wote. (MATHAYO 28:1-12) Atukuzwe Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu na ushirika wa Roho Mtakatifu kwa Ujumbe wa Msalabani ambao umetupatia ushindi dhidi Ibilisi,dhambi,laani, umaskini,magonjwa na udhaifu wa kila namna katika Jina la BWANA. #FAHAMU PIA:- #WAEBRANIA SURA YA 12: 1 Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu, tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu. 3 Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu. 4 Hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi 1WAKORINTHO SURA YA 11: 23 Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, 24 naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. #YOHANA SURA YA 3:14-18 14 Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye. Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. https://www.instagram.com/kongwastone/p/Bgy6oIMFAGg/?utm_source=ig_tumblr_share&igshid=1975lharvgn3