World NGO Day Siku ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Duniani. #sdgs #ngo https://www.instagram.com/p/B9FZwkeHhNI/?igshid=1xn1xemr8iz8
he wasn't even looking at me and he found me

roma★

Origami Around
2025 on Tumblr: Trends That Defined the Year

Kaledo Art

tannertan36
Cosmic Funnies

Product Placement
Claire Keane
Alisa U Zemlji Chuda
Peter Solarz

pixel skylines
todays bird
No title available
almost home

Discoholic 🪩
d e v o n
art blog(derogatory)
Aqua Utopia|海の底で記憶を紡ぐ

No title available
seen from United States
seen from T1

seen from Taiwan

seen from Indonesia

seen from United States

seen from Netherlands

seen from United States
seen from Brazil

seen from Malaysia

seen from United States
seen from United States

seen from Maldives
seen from United States

seen from United States
seen from United States
seen from Germany
seen from Türkiye
seen from Italy
seen from United States

seen from Singapore
@kataarushwatz
World NGO Day Siku ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Duniani. #sdgs #ngo https://www.instagram.com/p/B9FZwkeHhNI/?igshid=1xn1xemr8iz8
Kurasa yetu mpya itakayojikita katika kutoa elimu ya maadili ili kutokomeza rushwa na kuleta maendeleo nchini. Tufuatilie @elimuadili Ahsante! https://www.instagram.com/p/B895Vi2nvVd/?igshid=km4guvlvpyai
KIGALI, RWANDA MAJAJI wanne nchini Rwanda wamehukumiwa vifungo jela baada ya kutiwa hatiani kwa kuhusika na vitendo vya rushwa, huku wengine 26 kesi zao zikiendelea na uchunguzi. Kwa mujibu wa idara ya uchunguzi nchini Rwanda, ilieleza kuwa kufunguliwa kesi, kushitakiwa hadi kufungwa kwa majaji hao kunaonesha jinsi gani nchi hiyo ilivyopabia kukabiliana na tatizo la rushwa. Mkuu wa Idara ya uchunguzi nchini humo, Jeannot Ruhunga alisema vita dhidi ya rushwa nchini Rwanda ni endelevu na kwamba hakuna ofisa wa ngazi yoyote atakyesalimika endapo atakayebainika kujihusisha na vitendo vya rushwa. Akizungumza katika mkutano wa mashauriano wa kuangalia mikakati ya kupambana na rushwa, Jeannot Ruhunga alisema mbali ya majaji hao kufungwa kwa rushwa pia mtumishi mmoja wa mahakama katika kitengo cha urajisi naye amehukumiwa kifungo jela. “Taarifa za kufungwa kwa majaji zimewashangaza wananchi wengi kwa sababu wanadhani kwamba majaji kwa hadhi zao hawawezi kula rushwa, lakini rushwa ni hulka ya binaadam, lakini viungo hivi vinaonesha kwamba tumedhamiria kukabilina na tatizo hili”, alisema. Kwa upande wake mmoja wa wataalamu wa shera nchini Rwanda, Anastase Murekezi alisema rushwa katika mahakama haihusishi mtu mmoja kwani huanzia kwa wanasheria, kwa warajis wa mahakama na mwishowe humfikia jaji. “Huu ni mnyororo na ni vigumu kuukata kwa sababu unapombana mmoja wengine husimama kumtetea yule aliyeshikwa hata kuwasilisha ushahidi wa uongo”, alisema Murekezi. #rwanda #kagame #judges #law #legal #court #change #activism #nonprofit #dogood #changemakers #DoSomething #humanity #SM4NP #impact #sustainability #sdgs #globalgoals #development #goals #corruption #sustainabledevelopment #kataarushwa #stopcorruption https://www.instagram.com/p/B8fjG4enERc/?igshid=1h0owapmyytoo
Mahakama ya juu ya Pietermaritzburg nchini Afrika Kusini imetoa hati ya kukamatwa kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma baada ya kushindwa kufika mahakamani kukabiliana na mashtaka kuhusu rushwa dhidi yake. Hati hiyo itafanya kazi ikiwa atashindwa kuhudhuria kesi yake itakayoanza mwezi Mei. Bwana Zuma anakabiliwa na makosa 16 ya kughushi, rushwa , ulaghai na utakatishaji fedha ukihusisha biashara ya silaha ya thamani ya mabilioni ya dola iliyofanywa tangu miaka ya 1990. Rais huyo wa zamani amefanikiwa kukwepa shutuma za rushwa dhidi yake kwa zaidi ya miaka 10. Lakini leo, sheria haikuwa upande wake. Hati ya kukamatwa kwake imetolewa baada ya kushindwa kufika mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi yake. Jopo la wanasheria wake waliwasilisha nyaraka wakisema kuwa mteja wao alikuwa mgonjwa na amekuwa akipatiwa matibabu nje ya Afrika Kusini tangu mwezi uliopita. Jaji Dhaya Pillay alihoji maelezo yaliyo kwenye nyaraka za matibabu za Zuma zilizowasilishwa na mawakili wake mahakamani. Lakini rais huyo wa zamani atakamatwa ikiwa atashindwa kufika mahakamani tarehe 6 mwezi Mei kesi yake itakapoanza rasmi. Bwana Zuma anakabiliwa na mashtaka kadha wa kadha ya rushwa ikihusisha malipo 783 yenye utata anayodaiwa kupokea kutoka kwa aliyekuwa mshauri wake wa masuala ya fedha Schabir Shaik. Madai hayo pia yamerejelea mkataba wa silaha uliofanyika miaka ya 1990 na kampuni moja ya masuala ya ulinzi ya nchini Ufaransa. #volunteers #causes #donate #change #activism #nonprofit #dogood #charity #fundraising #philanthropy #SocialGood #changemakers #DoSomething #humanity #SM4NP #impact #sustainability #sdgs #globalgoals #development #youth #agenda #goals #sustainabledevelopment #kataarushwa #stopcorruption https://www.instagram.com/p/B8O9X4MnS7J/?igshid=1mnhm31oqm0oe
TAASISI Ya Kuzuia Na Kupambana Na Rushwa TAKUKURU Mkoa Wa Morogoro Imesema Imeweza Kuokoa Kiasi Cha Shilingi Milioni Tisini Na Sita Thelathini Na Tano Elfu Mia Tisa Thelathini Na Mbili Kwa Njia Ya Point Of Sale (POS) Ambazo Zilikua Hazijawasilishwa Kwa Wakati Katika Akaunti Za Mapato Za Halmashauri. Hayo Yamesemwa Na Naibu Mkuu Wa TAKUKURU Mkoa Wa Morogoro Victor Swella Wakati Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Januari 22, 2020 Akitoa Taarifa Ya Kazi Zilizotekelezwa Na TAKUKURU Katika Kipindi Cha Miezi 3 Kuanzia Octoba Hadi Desemba 2019. Swella Amesema Mashauri Yanayohusiana Na Ubadhilifu Wa Makusanyo Kwa Njia Ya POS Yalifanywa Na Watumishi Katika Halmashauri Za Wilaya Za Ulanga Na Kilombero Yamefunguliwa katika mahakama ya za wilaya za ulanga na kilombelo ambapo kesi ECO17/2019 imefunguliwa katika mahakama ya Kilombrlo na ECO23/2019 katika mahakama ya Ulanga Katika Ufuatiliaji Wa Maendeleo Amesema Ufuatiliaji Ulifanyika Katika Miradi Inayoendelea Chini Ya Mpango Wa Serikali Za Mitaa Wa Kuendeleza Miji Ambayo Ni Mradi Wa Ujenzi Wa Soko Kuu wenye thamani ya shilingi bilioni kumi na saba milioni mia sita hamsini na tano mia nane thelethini na tatu elfu mia nne na tano na seti sitini na tano(17,655,833,405.65/=). Ujenzi Wa Kituo Cha Daladala Kaloleniwenye thamani ya shilingi milioni sabini na ishirini na nne mia saba sitini na mbili elfu mia tano(724,762,500/=), Mradi Wa Stendi Ya Mafiga wenye thamani ya shilingi bilioni tano milioni mia mbili na arobaini na saba mia tatu themenini na tano elfu mia tisa arobaini na senti arobaini na tisa( 5,247,385,940.490 Na mradi mwingine ni ule wa Ujenzi Wa Mtaro Mkubwa Uliopo Eneo La Kikundi wenye thamani ya shilingi milioni mia saba sabini na nne na elfu sita mia tano(774,006,500) Aidha Takukuru Imetoa Wito Kwa Wagombea Pamoja Na Wapambe Waomwanaoanza Kucheza Rafu Mapema Kwa Kufanya Kampeni Za Chini Kwa Chini Hususani Kuwahonga Wananchi Kwa Lengo La Kuwarubuni Ili Waweze Kuwachagua Kipindi Uchaguzi Mkuu Utakapofika. #volunteers #causes #donate #change #activism #nonprofit #dogood #charity #fundraising #philanthropy #sustainability #sdgs #globalgoal #uchaguzi #morogoro #takukuru https://www.instagram.com/p/B7rHgkanoeq/?igshid=x6fefi0pce5v
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Shinyanga imeokoa Shilingi milioni 30, laki tano na elfu tatu miasita na hamsini kutoka kwa Viongozi wa Vyama vya ushirika (AMCOS) waliofanya ubadhirifu wa Fedha za Wakulima wa Pamba msimu wa Mwaka 2018/2019. Akizungumza na waandishi wa habari januari 14 mwaka huu Kaimu Mkuu wa (TAKUKURU) Mkoa wa Shinyanga, Hussein Mussa alisema kuwa ofisi yake ilifuatilia kwa kina madeni ya Wakulima wa Pamba wanaodai fedha zao kutokana na pamba waliyouza kupitia AMCOS na kubaini kuwepo ubadhilifu wa fedha za wakulima. Alisema kuwa Baada ya uchunguzi TAKUKURU ilibaini kuwa AMCOS saba za Lugana, Mwakipoya, Ng'washinong'hela, Nyenze, Kalitu, Kweli Balimi na Ibadakuli ndizo zinadaiwa fedha na wakulima wa pamba shilingi 109,497,130 licha kuwa fedha hizo zimekwisha kutolewa na Kampuni za Ununuzi. “TAKUKURU ilibaini kuwa mpaka kufikia mwezi Desemba 2019 makampuni yaliyonunua pamba mkoani Shinyanga yalikuwa hayadaiwi Fedha za Wakulima bali walikuwa yanadaiwa ushuru wa AMCOS jumla ya Shilingi 890,105,580 alisema Mussa. Amefafanua kuwa kuwa baada ya kubaini ubadhirifu huo Takukuru iliweza kuwakamata baadhi ya Viongozi wa AMCOS waliofanya ubadhilifu wa fedha za Wakulima na waliweza kurejesha kiasi cha Shilingi 30,503,650 fedha ambazo zinatarajiwa kugaiwa kwa Wakulima hivi Karibuni. “ Viongozi wa AMCOS ya Kweli Balimi ya Wilaya ya Shinyanga ambao walirejesha Fedha walizokuwa wanadaiwa kiasi cha Shilingi 6,362,400 walikuwa wamezifanyia ubadhilifu na tayari fedha hizo zimeshatolewa kwa Wakulima” alisema Mussa. Aliwataka wananchi wa Mkoa wa Shinyanga wametakiwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU ili Kuhakikisha wanatokomeza rushwa katika mkoa wa Shinyanga. #volunteers #causes #donate #change #activism #nonprofit #dogood #charity #fundraising #philanthropy #SocialGood #changemakers #DoSomething #humanity #SM4NP #impact #sustainability #sdgs #globalgoals #development #youth #agenda #goals #sustainabledevelopment #kataarushwa #stopcorruption https://www.instagram.com/p/B7dVeGFnFvY/?igshid=r6tuz2n8pzdi
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa Taasisi ya Kuzua na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ukamilishe mapema uchunguzi dhidi ya madudu yaliyoibuliwa katika mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 na wizi uliofanywa na viongozi wa AMCOS kwa wakulima wa ufuta na korosho ikiwemo wilaya ya Ruangwa. Ameyasema hayo leo wakati akizindua jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Ruangwa lililogharimu zaidi ya sh. milioni 142. Ametoa wito kwa TAKUKURU kuwa imara na kuweza kutembea kifua mbele katika mapambano hayo. Waziri Mkuu amesema pamoja na TAKUKURU kuendelea na utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku pia ameuagiza uongozi wa taasisi hiyo ukamilishe mapema utekelezaji wa maagizo mbalimbali ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyoyatoa kwao kwa nyakati tofauti. Amesema ameshuhudia kazi nzuri waliyoifanya na wanayoendelea kuifanya kupitia uchunguzi na ufuatiliaji wa madai ya malipo ya wakulima wa zao la ufuta na korosho.“Kamilisheni chunguzi hizi zote kwa wakati ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya wale wote waliopatikana na hatia.” Amesema rushwa huathiri utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. “Kutokana na ukweli huo, Serikali imetoa msukumo wa pekee katika kushughulikia vitendo vya rushwa na ufisadi. Msukumo huo, umechangia kwa kiasi kikubwa hususan katika kipindi hiki, utekelezaji wa miradi mikubwa na ya kimkakati kwa ufanisi na kwa wakati.” Amesema wananchi wanatakiwa wafahamu kwamba kwamba nchi yoyote ambayo rushwa imetamalaki siyo rahisi kuwa na uwezo wa kiuchumi utakaoiwezesha nchi hiyo kumudu kulipa madeni ya ndani na ya nje. “Hata hivyo, kwa upande wa Tanzania tunashuhudia jinsi Serikali ya awamu ya tano inavyolipa madeni.” #volunteers #causes #donate #change #activism #nonprofit #dogood #charity #fundraising #philanthropy #SocialGood #changemakers #DoSomething #humanity #SM4NP #impact #sustainability #sdgs #globalgoals #development #youth #agenda #goals #sustainabledevelopment #kataarushwa #stopcorruption https://www.instagram.com/p/B7dFKZ_H1e1/?igshid=1usu0kp8tt7xl
Mmomonyoko wa maadili na Migongano ya maslahi kwa Viongozi kwa baadhi ya viongozi wa mashirika na taasisi za Umma mkoani Shinyanga umetajwa kusababisha hasara kwa serikali kutokana na uwepo wa ufanisi mdogo katika usimamizi wa miradi ya maendeleo. Hayo yalibainishwa Januari 10 mwaka huu na Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela wakati akifungua mafunzo ya siku mmoja ya sheria ya maadili yaliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kujumuisha watendaji wakuu wa taasisi na mashirika ya Umma. Alisema kuwa Sheria ya maadili ya Viongozi wa Umma inaelekeza majukumu ya viongozi wa taasisi na mashirika ya Umma, kusimamia sheria za Nchi, haki na utu ili kumsaidia Rais katika kutekeleza majukumu yake na hatimaye kutoa huduma bora kwa jamii na kuepuka kujiingiza katika migogoro isiyokuwana tija. “Wapo baadhi ya viongozi wa Umma wanaendekeza migogoro kwenye maeneo yao yakazi kwa kufanya kazi kwa makundi na kusababisha watumishi kutowajibika ipasavyo kinyume na viapo vyao,kama wapo humu hebu wajirekebisheni haraka kabla hatua za kinidhamu hazijachukuliwa dhidi yao, alisema Msovela. Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kanda ya Magharibi inayojumisha mikoa ya Tabora,Shinyanga,Simiyu na Kigoma,kutoka Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma, Gerald Mwaitebele alisema kuwa endapo viongozi hao wataamua kubadilika malalamiko hayatajitokeza tena na wananchi watapata huduma za kijamii vizuri. “Tangu tumeanza kutoa mafunzo haya katika mikoa yetu ya kanda ya magharibi tumeona mabadiliko makubwa hususani suala la maadili, uadilfu na vitendo vya rushwa limepungua na kutupa matumaini ya kuendelea kutoa elimu hii kwa ngazi zote kwenye jamii kama vile shuleni na kwenye mikutano ya hadhara ya vijji na mitaa” alisema Mwaitebele. #volunteers #causes #donate #change #activism #nonprofit #dogood #charity #fundraising #philanthropy #SocialGood #changemakers #DoSomething #humanity #SM4NP #impact #sustainability #sdgs #globalgoals #development #youth #agenda #goals #sustainabledevelopment #kataarushwa #stopcorruption https://www.instagram.com/p/B7dExiqnBmE/?igshid=yc9iljs37f7c
Wataalam tarajali wa kada mbalimbali katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila wamepatiwa mafunzo elekezi lengo ikiwa ni kuwaelekeza maadili mema ya utumishi wa umma mahala pa kazi Akitoa mada katika mafunzo hayo Afisa Mwandamizi kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Bi. Heavenlight Majule amesema maadili mema ndio msingi utakaowawezesha kufanya kazi kwa ufanisi. “Ukosefu wa maadili mahala pa kazi umepelekea haki za watu kupotea kutokana na kukithiri kwa vitendo vya rushwa ambavyo vimepelekea watoa huduma kutoa huduma zilizo chini ya viwango” amesema Bi. Majule. Aidha ametaja vyanzo mbalimbali vya mmomonyoko wa maadili ambavyo vinaathiri mienendo ya watumishi wa uuma kuwa ni pamoja na tamaa yaani kutoridhika na kile wanachokipata kwa mwajiri, ubinafsi, muundo wa maisha na aina ya marafiki. Kwa upande wake Afisa Maadili kutoka Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Bw. Hamadi Bakari amesisitiza kuwa maadili mema ni pamoja na kutoa huduma bora, utii kwa Serikali, bidii ya kazi, huduma bila upendeleo, uadilifu, uwajibikaji, kuheshimu matakwa ya sheria pamoja na matumizi sahihi ya taarifa. “Maadili mema ni kufanya kilicho sahihi ambapo imeainisha katika kanuni ya 65 ya maadili ya utendaji katika utumishi wa Umma ya marekebisho ya mwaka 2005 inayoelezea sifa za mtumishi mwadilifu” amesema Bw. Bakari. Awali akizungumza na tarajali hao Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya MNH-Mloganzila Dkt. Mohamed Mohamed amewasisitiza wataalam tarajali kuwa mafunzo wanayopatiwa hospitalini hapa yawasaidi katika kufanya kazi kwa utii na uadilifu. Mada zilizowasilishwa katika mafunzo hayo ni pamoja na elimu elekezi ya kuzuia na kupambana na rushwa mahali pa kazi, huduma mbalimbali zinazotolewa hospitalini hapa, mafunzo ya masuala ya ukimwi mahala pa kazi, maadili ya utumishi wa umma na kanuni za kazi. #volunteers #causes #donate #change #activism #nonprofit #dogood #charity #fundraising #philanthropy #SocialGood #changemakers #DoSomething #humanity #SM4NP #impact #sustainability #sdgs #globalgoals #development #youth #agenda #goals #sustainabledevelopment #kataarushwa #stopcorruption https://www.instagram.com/p/B7dEk7QH_Ld/?igshid=1bim12q2dgpu8
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, ameiagiza Menejimenti ya Wizara ya Fedha na Mipango kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wahasibu wote wanaofanya vitendo vinavyokinzana na maadili ya kitaaluma ya uhasibu kama wizi, ubadhirifu wa mali za umma, ufisadi na rushwa. Dkt. Mpango alitoa maagizo hayo wakati akifungua Kikako Kazi cha kuandaa Hesabu za Majumuisho za Serikali za mwaka 2018/19 pamoja na kuzindua Mfumo mpya wa uandaaji wa taarifa za fedha za Majumuisho (Government Accounting Consolidation System (GACS), Jijini Dar es Salaam Dkt. Mpango aliwataka wahasibu wote nchini kuwa wazalendo na kusimamia ipasavyo matumizi ya rasimali za Umma na kuwataka kuhakikisha kuwa usalama katika Mifumo ya Fedha unakuwa madhubuti ili kuondoa uwezekano wa mifumo hiyo kudukuliwa na kuleta hasara kubwa kwa Serikali na Wananchi. Aidha Dk. Mpango alimpongeza Mhasibu Mkuu wa Serikali CPA Francis Mwakapalila, pamoja na Mkurugenzi wa Mifumo ya Fedha Bw. John Sausi kwa kuonesha dhamira na nia ya kweli ya kuhakikisha wanatengeneza Mifumo bora ya kifedha ili kuleta ufanisi mkubwa katika kukusanya na kuhasibu mapato na matumizi ya Serikali. Aliongeza kuwa dhamira hiyo imedhihirika kwa kuanzisha Mifumo ya Kifedha ya kimtandao kama Government e-payment Gateway (GePG), Government Salary Payment Platform (GSPP), na sasa Government Accounting Consolidation System (GACS). ‘’Nimefurahi sana kuona kwamba ndani ya kipindi kifupi cha miaka minne tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, mmeanzisha Mifumo mingi na madhubuti ya kukusanya Mapato na Maduhuli ya Serikali, pamoja na Mifumo ya kuhasibu rasilimali za umma yenye kukidhi viwango vya kimataifa” alisema Dkt. Mpango. Pia alieleza kuwa matarajio ya Serikali ni kwamba mfumo huu ulioanzishwa pamoja na Mifumo iliyokwisha kuanzishwa itaitumika vizuri kwa weledi na uadilifu mkubwa katika kutoa huduma bora kwa Wananchi na ikizingatiwa hilo matarajio ya wananchi na rasimali za umma zitatumika ipasavyo kuboresha Maisha yao. #volunteers #causes #donate #change #activism #nonprofit #dogood #charity #fundraising #philanthropy #SocialGood #changemakers #DoSomething #humanity #SM4NP #impact #sustainability #sdgs https://www.instagram.com/p/B7dD8ayn0J1/?igshid=1qz61xf9tuabz
Watu watano wakiwamo wanaodaiwa kuwa askari polisi wawili wa kituo cha Himo mkoani Kilimanjaro wanatuhumiwa kumteka mfanyabiashara wa mjini Moshi na kumbambikia tuhuma kisha baadaye kumwomba rushwa ya Sh140 milioni. Baada ya kumkamata, watu hao ambao awali inadaiwa walijitambulisha kama maofisa wa idara ya usalama wa Taifa, walizunguka na mfanyabiashara huyo kwa mawakala wa Benki ya CRDB ili atoe fedha hizo. Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa Kilimanjaro, James Manyama alipoulizwa juzi alikiri kuwapo kwa malalamiko hayo lakini akasema suala la polisi wanaotajwa kuhusika, litashughulikiwa kiutawala. Taarifa zaidi zinaeleza kuwa askari hao walikubali wapewe Sh30 milioni baada ya kujadiliana kwa saa kadhaa kutokana na awali kutaka Sh140 milioni baada ya kumtisha mfanyabiashara huyo kuwa anakwenda kushitakiwa kwa kosa la utakatishaji fedha. Awali gazeti hili lilimtafuta Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Salum Hamduni ambaye alisema hajapewa taarifa hizo na kuahidi kufuatilia baada ya mwandishi wetu kumpa namba ya jalada. Suala hilo limefunguliwa jalada namba MOS/RB/79/2020 katika kituo kikuu cha Polisi mjini Moshi ambapo polisi wawili wa kituo cha Himo walitambuliwa na mlalamikaji wakiwa ni miongoni mwa watu watano wanaodaiwa kumteka. #volunteers #causes #donate #change #activism #nonprofit #dogood #charity #fundraising #philanthropy #SocialGood #changemakers #DoSomething #humanity #SM4NP #impact #sustainability #sdgs #globalgoals #development #youth #agenda #goals #sustainabledevelopment #kataarushwa #stopcorruption https://www.instagram.com/p/B7dDgI4HvFT/?igshid=1tgicj95vogfw
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewatahadharisha vijana Nchini kuwa macho na Watu walioanza kufanyakazi kinyemela katika mchakato wa kujipanga katika kujiandaa kugombea nafasi za Uongozi kwenye Uchaguzi Mkuu hapo baadae Mwaka huu. Alionya kwamba vitendo vinavyoashiria dalili za kufanywa na Watu hao vieleweke kwamba ni kinyume na taratibu zilizowekwa na Taifa na hata Vyama wa Kisiasa kwa vile wakati wa kufanya hivyo haujafika wala kutangazwa rasmi. Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa alitoa tahadhari hiyo wakati akizindua Matembezi ya Umoja wa Vijana wa CCM {UVCCM} katika kusherehekea Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyoanzia katika Kijiji cha Kizimkazi Dimbani Mkoa wa Kusini Unguja. #volunteers #causes #donate #change #activism #nonprofit #dogood #charity #fundraising #philanthropy #SocialGood #changemakers #DoSomething #humanity #SM4NP #impact #sustainability #sdgs #globalgoals #development #youth #agenda #goals #sustainabledevelopment #kataarushwa #stopcorruption https://www.instagram.com/p/B63vV21nraW/?igshid=11k2u61qnzseo
MVUA zinazoendelea kunyesha kwa wingi katika wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma,zimesababisha kuharibika kwa miundombinu ya barabara katika mtaa wa Kipika kata ya Matarawe wilayani humo na hivyo kutishia kukata mawasiliano kati ya mtaa huo na maeneo mengine ya mji wa Mbinga. Kutokana na uharibifu uliotokea,baadhi ya wakazi wa mji wa Mbinga wameiomba Serikali kuwachukulia hatua ikiwemo kuwafikisha mahakamani makandarasi na wahandisi wa wakala wa barabara vijijini na mijini Tanzania (TARURA) kwa kushindwa kusimamia majukumu yao ikiwemo ujenzi wa mradi huo chini ya kiwango. Walisema, ni kawaida baadhi ya barabara katika mji wa Mbinga kuharibika ndani ya muda mfupi tangu zinapojengwa na hali hiyo inatokana na wahandisi kushindwa kutumia taaluma zao wakati wa kutekeleza miradi ya Barabara katika wilaya hiyo. Wamesema, kupeana kazi za ujenzi wa miradi ya barabara kwa misingi ya urafiki na kujuana kwa kiasi kikubwa kumechangia miradi mingi ya barabara katika mji huo kujengwa chini ya kiwango na hivyo kushindwa kuleta tija. Aidha,wameiomba taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza mikataba inayoingiwa kati ya Tarura na Makandarasi ili kufahamu juu ya uwezo wa wakandarasi wanaopewa kazi katika Mji wa Mbinga. Wakiongea kwa nyakati tofauti,wakazi hao Antonia Komba,Daud Shija na Suzana Ndomba wamesema, baadhi ya miradi inayojengwa haimalizi kero za wananchi licha ya kutekelezwa kwa fedha nyingi za walipa kodi wa nchi hii. Antonia Komba mkazi wa mtaa huo, alitolea mfano ujenzi wa mifereji iliyojengwa katika barabara ya Kipika mtaa wa Kipika imedumu kwa miezi saba tu tangu ilipojengwa na sasa imeharibika kutokana na kusombwa na maji ya mvua na hivyo kushindwa kumaliza kero ya muda mrefu ya wananchi wa kata ya Matarawe. #volunteers #causes #donate #change #activism #nonprofit #dogood #charity #fundraising #philanthropy #SocialGood #changemakers #DoSomething #humanity #SM4NP #impact #sustainability #sdgs #globalgoals #development #youth #agenda #goals #sustainabledevelopment #kataarushwa #stopcorruption https://www.instagram.com/p/B63uChSneE8/?igshid=vfnknllft7gk
Imeelezwa kwamba, Ukiukwaji wa maadili, upendeleo, ubinywaji wa maslahi ya watumishi na watumishi kutopewa nafasi ya kutoa mawazo yao, ni baadhi ya mambo yanayoweza kupelekea uwapo wa vitendo vya kutoa na kupokea rushwa sehemu ya kazi. Hayo yameelezwa leo (Ijumaa) na Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Bw. Joseph Mwaisalo, wakati alipokuwa akitoa mafunzo kuhusu uzuiaji na kupambana na rushwa kwa Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Mafunzo hayo na ambayo yalifunguliwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, DkT. Evaristo Longopa,yamewahusisha watumishi wote kuanzia Wakurugenzi wa Idara, Wakurugenzi Wasaidizi, Wakuu wa Vitengo, Mawakili wa Serikali na watumishi wa Kada Mbalimbali waliopo Jijini Dodoma. “ Rushwa ni zaidi ya hongo”. Anasema Bw. Joseph Mwaisalo. Na kuongeza. “Rushwa ni mmomonyoko wa maadili, mtumishi anaponyimwa haki yake ya kupandishwa cheo, au stahili yoyote ile ambao ni haki yake inatengeneza mazingira ya rushwa. Na kwa sababu hiyo, amewataka watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali siyo tu kuhakikisha wanazuia uwepo wa mianya ya utoaji na upokeji wa rushwa lakini ni vizuri kwao pia kuzitambua haki zao, kuzidai kwa misingi ya sheria, taratibu na kanuni na kwa Menejimenti kuhakikisha kwamba inazingatia maslahi ya watumishi wake. Akasema, watumishi wengi na hata wananchi waliowengi hawazijui haki zao na namna halali ya kuzidai haki zao na ndio maana wengi wao wanaishia kuombwa rushwa ikiwamo rushwa ya ngono. “Rushwa ipo kila mahali, hata hapa katika Ofisi ya Mwanasheria kunauwezekano wa kuwapo kwa mazingira ya rushwa kupitia utekelezaji wa majukumu yenu hasa mkizingatia kwamba hii ni Taasisi nyeti sana na ambayo ni mdau wetu mkubwa katika mapambano dhidi ya rushwa”. Anasisitiza Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma. Akasema kutokana na unyeti wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na umuhimu wake kwa Taifa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jeneral John J. Mbungo, ameguswa sana na uamuzi wa Taasisi hii muhimu wa kuwa na mafunzo haya ya kuelimishna juu ya kuzuia na kupambana na rushwa kwa watumishi wake. #volunteers #causes #donate #change https://www.instagram.com/p/B63qSrSncny/?igshid=4dww1lhb6whm
MAHAKAMA ya Angola imeagiza kukamatwa kwa mali na akaunti za benki za bilionea ambaye ni binti wa rais wa zamani wa Angola, Jose Eduardo Dos Santos, Bi Isabel Dos Santos. Kukamatwa kwa mali hizo kunatokana na mipango ya serikali iliyopo kukabiliana na ufisadi katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta. Utawala wa Rais Joao Lourenco unataka kuchukua takriban dola bilioni moja ambazo umekuwa ukimdai Bi Isabel Dos Santos na washirika wake. Amepinga madai hayo na kusema kwamba hajafanya makosa yoyote wakati babake alipokuwa mamlakani. Akidaiwa kuwa mwanamke tajiri zaidi barani Afrika, Bi Dos Santos anakadiriwa na jarida la Forbes kuwa na mali yenye thamani ya dola bilioni 2.2. Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 46 anaishi ughaibuni, akisema kwamba aliondoka Angola kwa kuwa maisha yake yalitishiwa. Anaendesha biashara kubwa akiwa na kampuni nchini Angola na Portugal ambapo anamiliki hisa katika kampuni ya Nos SGPS. Mahakama iliagiza mali ya Bi Santos kupigwa kuchukuliwa ikiwemo akaunti zake za benki mbali na hisa zake katika kampuni nchini Angola, ikiwemo ile ya Unitel na Benki ya Fomento de Angola (BFA) kilisema chombo kimoja cha habari cha serikali ambapo naye alisema anashutumu kile alichokitaja kuwa shambulio linaloshinikizwa kisiasa. #volunteers #causes #donate #change #activism #nonprofit #dogood #charity #fundraising #philanthropy #SocialGood #changemakers #DoSomething #humanity #SM4NP #impact #sustainability #sdgs #globalgoals #development #youth #agenda #goals #sustainabledevelopment #kataarushwa #stopcorruption #angola #isabeldossantos #dossantos https://www.instagram.com/p/B6zRahznDpE/?igshid=arrdr0fvaflw
Asasi za kiraia na mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoani Shinyanga yametakiwa kutobatilisha matumizi ya fedha wanazopatiwa na wahisani mbalimbali kutoka nje ya nchi na badala yake wazilekeze katika malengo mahususi ili kuleta tija na mabadiliko chanya katika jamii wanazozihudumia. Hayo yamebainishwa na Kaimu mkuu wa kanda ofisi ya Rais, Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, Gerald Mwaitebele, wakati akitoa mafunzo kwa viongozi wa asasi mbalimbali kuhusiana na sheria ya maadili ya viongozi wa Umma yaliyofanyika mjini Shinyanga. “Wapo baadhi ya viongozi wa mashirika na asasi hizi hubatilisha matumizi ya fedha wanazopatiwa na wahisani hususani fedha za kulelea watoto yatima wazee,na makundi mengine katika jamii yasiyo jiweza lakini wapo watumishi wa umma waliokasimishwa majukumu ya kuzisimamia tutahakikisha hawajihusishi na rushwa”alisema Mwaitebele. Sheria ya maadili ya viongozi wa umma inakataza viongozi wa asasi hizi kujinufaishwa wenye kuwa kutumia mamlaka yao vibaya ikiwa ni pamoja kutumia fedha za wahisani katika shughuli zao binafsi jambo ambalo litanaweza kuwakatisha tama wafadhili wao na kuipa sifa mbaya kuhusiana na asasi na mashirika haya. “Kila kiongozi wa asasi na mashirika yasiyo ya kiserikali anawajibu wa kuhakikisha ana timiza malengo mahususi kwa kuzingatia katiba zao za undeshaji wao ili kuepuka migongano ya maslahi baina yao na jamii wanayoihudumia”alisema Doto. Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya viongozi wa asasi hizo,Mericiana Stanley katibu mkuu wa taasisi ya Young Women Christian Asociasion (YWCA) na Joseph Mpagala mkurugezi wa Asasi ya (COWOSE) za mkoani Shinyanga walisema wameipongeza tume ya maadili kwa kutoa mafunzo hayo kwani yamesaidia kuwakumbusha wajibu wao katika utendaji kazi. Wamesema endapo viongozi wa umma ambao wamepewa mamla ya kuzisiamia asasi na mashirika hayo kwa weledi vitendo vya rushwa na ubatilishwaji wa fedha za wahisani hautajitokeza pindi wanapopata misaada mbalimbali kutoka kwa wahisani wao kwaajili ya kuihudumia jamii. #volunteers #causes #donate #change #activism #nonprofit #dogood #charity #fundraising #philanthropy #SocialGood #changemakers #DoSomething https://www.instagram.com/p/B6zQb71HmN7/?igshid=161wuazongug1
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amekemea matukio ya vitendo vya ukatili wa kijinsia katika Vyuo vya elimu ya juu hasa vitendo vya rushwa ya ngono. Dkt. Jingu ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akifungua kikao kilichowakutanisha Wakuu wa vyuo vya elimu ya juu kilichohusu namna ya kupambana na ukatili wa kijinsia katika maeneo ya Vyuo vya elimu ya juu. Dkt. Jingu ameongeza kuwa tatizo la ukatili wa kijinsia limekuwa likishamiri katika Vyuo vya elimu ya juu kwani imeripotiwa kuwa wahadhiri wengi wamekuwa wakitumia madaraka yao kuwalazimisha wanafunzi kufanya nao ngono kwa lengo la kuwafaulisha mitihani. Amesema kuwa sio wanafunzi pekee wanaokumbana na vitendo hivyo ila hata wafanyakazi wanaofanya kazi katika Vyuo vya elimu ya juu wanakubwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia hivyo nguvu ya ziada inahitajika katika kupambana na vitendo hivyo vyuoni. Dkt. Jingu amesema kuwa katika kuhakikisha tunapambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia Serikali na Wadau wanatekeleza Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na Watoto ili kuhakikisha kuwa vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia nchini vinatokomezwa kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2030. Aidha Dkt. Jingu amewataka wakuu wa vyuo hao kuhakikisha wanatoa elimu na maelekezo ili kujenga uelewa wa kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa kwa wanafunzi wa kike kwa kwa ajili ya kuepuka matakwa ya wahadhiri wanaotumia hila kuendekeza ukatili wa kingono vyuoni. Pia Dkt. Jingu amewataka Wakuu wa vyuo hao kuhakikisha wanatekeleza Agizo la Waziri Ummy Mwalimu la kuanzisha madawati ya jinsia katika vyuo vyao ili kuwezesha kuondokana na vitendo vya kikatili na kujenga mazingira yaliyosalama katika vyuo vyetu. Kwa upande wake Mkuu wa Uelimishaji kutoka Taasisi ya Kupambana na Kutokomeza Rushwa TAKUKURU Bw. Asseri Mandari amesema kuwa Taasisi hiyo imejipanga kupamabana na tatizo hilo kwa kuanzisha Kampeni inayaosema “Vunja Ukimya Ondoa Rushwa ya Ngono” itakayosaidia kuondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa kuzuia rushwa ya ngono. #sdgs #kataarushwa #stopcorruption #corruption https://www.instagram.com/p/B6b6ADSHgTw/?igshid=1qyptctxwtnhp