Mkongwe wa filamu kutoka hollywood Marekani, Will Smith hatimaye amefunguka kuhusiana na kashifa za uvaaji wa mavazi ya kike zinazomwandama mtoto wake wa kiume aitwaye jaden.
Akizungumza kwenye mahojiano aliyofanyiwa na kituo cha BBC1, Will alinukuliwa akisema ‘Jaden’ amekuwa akiamini kile anachokifanya katika sanaa yake ya mitindo licha kwa upande wao kama wazazi imekuwa ikiwaogopesha.
”Asilimia 100 Jaden sio muoga, yeye anaweza akafanya kitu chochote, tukiwa kama wazazi inatutisha, kweli inatishia. Lakini yeye yupo tayari kuishi na kufa kwa maamuzi yake mwenyewe kisanii, wala hajali watu wanamchukuliaje”, alisema Will
Aliongeza : ”Unaweza ukawa unajaribu vitu na kupenda kuendelea kuvifanya ambavyo jamii haikubaliani nayo, na unaweza ukawa huru kufanya vitu ambavyo unaweza ukavishindwa”.
Hatua hiyo imekuja kufuatia vyombo mbalimbali vinavyoandika habari hasa za udaku kummulika staa huyo wa The Karate Kid ambaye amekuwa akijihusisha na mitindo huku mavazi anayoyatumia kwenye sanaa yake yakipelekea jamii kumfikiria ndivyo sivyo.
WILL SMITH AJIBU TUHUMA NZITO ZINAZOMKABILI MTOTO WAKE WA KIUME Mkongwe wa filamu kutoka hollywood Marekani, Will Smith hatimaye amefunguka kuhusiana na kashifa za uvaaji wa mavazi ya kike zinazomwandama mtoto wake wa kiume aitwaye jaden.